Tabora hoi kielimu

Tabora hoi kielimu

kazikubwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2010
Posts
597
Reaction score
148
Shule ya Sekondari ya Kata ya Ndevelwa iliyopo mkoani Tabora imeweka historia kwa kuwa na wanafunzi watoro kupindukia. Form Four wamebaki wanafunzi 3 kati ya 36. Form Three yupo mwanafunzi 1 kati ya 30 waliosajiliwa. Form Two na Form One ni aibu kupindukia.

Diwani anasema sababu ni kuwaoza mabinti na maisha magumu. Ikumbukwe huu ndio msimu wa kulima Tumbaku sasa.

Lipumba, Sitta, Prof. Safari jahazi linazama nyumbani. Source ITV
 
hiyo ndo hali halisi ya vijiwe vyetu vinavyoitwa shule za kata,kule hakuna kitu ni kupotezeana muda tu watoto wanaona ni bora wakaendelee na maisha mengine.
 
alafu jaribu kuwashauri uone kama hawajakuroga .............huu mkoa ni balaa tupu
 
Huu mkoa inabidi ubadilike sasa. Yanahitajika mapinduzi makubwa ya kifikra huko Tabora
 
Back
Top Bottom