Tabora: Mashamba makubwa ya Tumbaku kupimwa

Tabora: Mashamba makubwa ya Tumbaku kupimwa

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729
1565719560396.png



Serikali imeuagiza uongozi wa mkoa wa Tabora kuhakikisha mashamba makubwa ya tumbaku yanapimwa.

Akizungumza na viongozi wa mkoa wa Tabora leo Jumanne Agosti 13, 2019, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania, Angelina Mabula amesema kwa kutopimwa mashamba hayo ina maana Serikali inakosa mapato.

Awali, mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amemweleza naibu waziri kuwa migogoro ya ardhi mkoani Tabora imepungua kwa kiwango kikubwa kutokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na mkoa pamoja na wilaya kwa kushirikiana na ofisi ya Ardhi kanda ya Magharibi.
 
Back
Top Bottom