Tabora mkoa kinara kwa wasiojua kusoma na kuandika

Tabora mkoa kinara kwa wasiojua kusoma na kuandika

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Nchini Professa Philipo Sanga amesema Mkoa wa Tabora ni kinara kwa asilimia kubwa ya watu wasiojua kusoma na kuandika katika mikoa mitano nchini ambayo bado ina changamoto hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya maonesho ya Kongamano la Kisomo Kimataifa na Jumuiya ya elimu ya watu wazima nchini linalofanyika Mkoa wa Katavi amesema ipo mikakati iliyoandaliwa ili kupambana na changamoto hiyo.

Katika takwinu hizo Mkoa wa Tabora unaongoza ukiwa na asilimia 32% ya watu wasiojua kusoma na kuandika ukifuatiwa na mkoa wa Katavi wenye asilimia 29.6% Mkoa wa Rukwa 26% Simiyu pamoja na mkoa wa Dodoma.

Amebainisha kuwa sababu kuu ni hali ya maisha na tamaduni za mikoa husika kwakuwa zinapakana kijiografia hivyo mkakati imewekwa ili kuhakikisha halmashauri husika katika mikoa zinasimamia vizuri ili kukabiliana na changamoto hiyo.
 
Ni nani katufikisha hapa kama Taifa, ndio alaumiwe.
Nadhani wenye mamlaka ndiyo wanapaswa kulaumiwa kwanza, halafu Sasa tunakuja Kwa mtu mmoja mmoja 🤔 au
 
Back
Top Bottom