TABORA: Mkoa wa Tabora nao Watangaza kumuunga mkono Lissu unakuwa mkoa wa 19 kutangaza azimio hilo

Rula ya Mafisadi

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2024
Posts
404
Reaction score
852
Your browser is not able to display this video.
===
Wakati zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi wa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wajumbe na viongozi wa chama hicho mkoa wa Tabora wameazimia kumuunga mkono mgombea wa nafasi hiyo Tundu Lissu, na kubainisha kuwa wanataka kiongozi mchapakazi kwa maendeleo ya chama hicho.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa CHADEMA Mkoa waTabora ,Yohana Lulyeho wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo ambapo amesema kuwa wameazimia kumuunga mkono Lissu wakiamini chama hicho kinahitaji mtu atakayeleta maendeleo ndani ya chama na mtu huyo ni Lissu.

Soma Pia: Simiyu: Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Chadema watangaza rasmi kumuunga mkono Tundu Lissu Uenyekiti Taifa, Wanakuwa ni Mkoa wa 17 sawa na 55% ya Mikoa yote


"Habari hizi za maridhiano na mapendano yaliyopo hazitaleta mabadiliko ya kisiasa kwenye nchi yetu, kwa hiyo tunahitaji kiongozi kama ambavyo katiba yetu imesema mara kadhaa, mwenye msimamo thabiti ambaye hawezi akayumbishwa na maneno ya pipi pipi, na kwa hali ya chama chetu ilivyo kiongozi huyo ni Tundu lissu", wameeleza.
 
Tusubiri tarehe 21 yote yatajulikana mbivu na mbichi. hizi nyingine ni bwebwe tu
 
Very objective!.
P
 
Mbowe ameshindwa kabisa kusoma ALAMA za nyakati..si angefanya hata karesearch kadogo tu kama alivyofanya kwa Late Lowasa
 
Hakuna kura ya mkoa bali kura ni ya mjumbe.

Msitujazie pumba hapa. Kama Lissu anashinda kama mnavyotuaminisha msingetumia nguvu nyingi kwenye mitandao kumtangaza hapa kila siku.

Subiri Jumanne 21/ 01 mtakavyoshangazwa na Mbowe. Mtalia kilio cha mbwa koko mdomo wazi meno nje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…