Rula ya Mafisadi
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 404
- 852
Wakati zikiwa zimesalia siku chache kuelekea uchaguzi wa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wajumbe na viongozi wa chama hicho mkoa wa Tabora wameazimia kumuunga mkono mgombea wa nafasi hiyo Tundu Lissu, na kubainisha kuwa wanataka kiongozi mchapakazi kwa maendeleo ya chama hicho.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa CHADEMA Mkoa waTabora ,Yohana Lulyeho wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo ambapo amesema kuwa wameazimia kumuunga mkono Lissu wakiamini chama hicho kinahitaji mtu atakayeleta maendeleo ndani ya chama na mtu huyo ni Lissu.
Soma Pia: Simiyu: Wajumbe Wa Mkutano Mkuu Chadema watangaza rasmi kumuunga mkono Tundu Lissu Uenyekiti Taifa, Wanakuwa ni Mkoa wa 17 sawa na 55% ya Mikoa yote
"Habari hizi za maridhiano na mapendano yaliyopo hazitaleta mabadiliko ya kisiasa kwenye nchi yetu, kwa hiyo tunahitaji kiongozi kama ambavyo katiba yetu imesema mara kadhaa, mwenye msimamo thabiti ambaye hawezi akayumbishwa na maneno ya pipi pipi, na kwa hali ya chama chetu ilivyo kiongozi huyo ni Tundu lissu", wameeleza.