Tabora: Mkufunzi wa 'Sensa' akutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni

Tabora: Mkufunzi wa 'Sensa' akutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni

Binadamu kifo kinampata popote pale na Guest ni eneo tuu kama maeneo mengine unategemea mgeni alale stand na huku posho anapata...
 
Huyo Mkufunzi wa Sensa ni Me au Ke?

WARUMI 6:23.

"Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu."
Kwanini umemuhukumu?

Ukisikia nyumba ya kulala wageni basi unawaza ni ngono tu?

Kwani hakuna wageni wa mbali waweza kulala?

Huyu mtu alitoka Kaliua.

Binadamu jamani, utafikiri weee ni mtakatifu.

Na kufa kila mtu atakufa hata kama u mwema vipi
 
Bahati Msengi ambaye ni mkufunzi wa sensa amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni, Kata ya Kanyenye mkoani Tabora.

Mkufunzi huyo ambaye pia alikuwa afisa elimu kata ya Milambo, wilayani Kaliua mkoani humo, alihudhuria mafunzo ya siku 21 yaliyomalizika juzi Jumanne na kufungwa na mkuu wa mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian, katika Chuo Cha Ualimu Tabora.

Msengi alikutwa amefariki jana Jumatano Julai 27, 2022 saa nane mchana katika nyumba ya kulala wageni ya Wema.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao amesema tukio hilo ni kifo cha kawaida kama vifo vingine vinavyotokea hospitalini.

Naye jirani wa nyumba hiyo ya wageni, -aidi Ahmed amesema mkufunzi huyo hakuwa ametoka ndani tangu alipoingia kulala juzi na ndipo walipofika baadhi ya jamaa na ndugu walioangalia kupitia dirishani na kumuona amelala kifudifudi.

Amesema walimuita kwa muda mrefu bila mafanikio na kuamua kuuvunja mlango wa chumba na kumkuta akiwa amekwisha kufariki dunia.

Mmoja wa wageni waliolala katika nyumbani hiyo na kuomba hifadhi ya jina lake alisema mkufunzi huyo aliingia chumbani na kulala baada ya kusalimiana naye na alionekana kuwa mwenye afya njema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.com
 
"Bahati Msengi"...

Huo ubini wa 'Msengi'... Nimemkumbuka mzee Msengi pale Milambo High School - Tabora, mpishi mkuu maarufu pale skonga, back in the day.

R.I.P mkufunzi wa sensa.

-Kaveli-
 
ukute marehemu alikuwa na watoto wakubwa tu ilo neno Gesti litawapa mawazo sana akilini mwao
 
Kama wanasema alikuwa anafanya dhambi Ina maana kama kungekuwa na demu nadhani mlango ungekuwa wazi kwani huyo demu angetokea huo mlango, lakini kama umefungwa Kwa ndani maana yake alikuwa pekee labda kama ni vumbi la Kongo Kisha demu akawa hajatokea
 
Kama wanasema alikuwa anafanya dhambi Ina maana kama kungekuwa na demu nadhani mlango ungekuwa wazi kwani huyo demu angetokea huo mlango, lakini kama umefungwa Kwa ndani maana yake alikuwa pekee labda kama ni vumbi la Kongo Kisha demu akawa hajatokea
 
Mungu mwema ampokee katika uso wake na kumjalia raha ya milele.
 
Back
Top Bottom