Kila sehemu ni pamugu wala si Tabora tu, mimi nipo hapa jijini Dar na nakuambia amini usiamini usipochacharika lazima urudi kijijini, hali ni ngumu sana, nauli ya kwenda kibaruani juu, chakula juu, kodi ya nyumba juu, umeme juu, maji hayapatikani ni kununua kwa dumu sh. 250.
Nilitamani kulikimbia jiji kama wewe ila nikapiga akili nikaona kukimbia mji utoto, nikagangamala sasa hali kidogo afadhali. kama walivyokushauri wengine kaza msuri, kijana wa kiume ukifika miaka 18 hakuna kulialia - ushakua. Watakucheka watuu....