Tabora: Serikali yamsaka muuguzi aliyebaka mgonjwa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Wizara ya Afya inafuatilia sakata la muuguzi anayedaiwa kumbaka msichana mgonjwa na kisha kukimbia kusikojulikana.

Akizungumza na watumishi wa hospitali ya wilaya ya Igunga na viongozi wa sekta ya afya mkoa wa Tabora, Naibu katibu mkuu (Tamisemi-Afya), Dk Dorothy Gwajima alisema lengo ni kuona haki inatendeka.

“Pia lazima kurudisha heshima ya sekta hiyo na hospitali ya wilaya ya Igunga,” amesema.

Ameeleza kuwa anayedaiwa kufanya tukio hilo ni mtu mmoja na hawezi kuchafua sifa ya sekta nzima ya afya na kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya mhusika.
Akimzungumzia mtumishi mwingine wa hospitali hiyo, anayedaiwa kuomba rushwa ya Sh200,000 na kukamatwa na Takukuru ambapo ana kesi mahakamani,alisema hilo liwe funzo kwa watumishi wa sekta ya afya akisema hospitali sio pango la kuomba rushwa.

Ameonya kuwa watumishi wanapokabiliwa na mkono wa sheria kwa kufikishwa mahakamani inakuwa si mwisho kwani watakumbana na mabaraza yao ya kitaaluma pamoja na kiutawala.

Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, Revocatus Kuuli, alisema tayari amemsimamisha kazi muuguzi anayekabiliwa na kesi ya rushwa mahakamani, akisubiri sheria ichukue mkondo wake.

Kuhusu mtumishi anayedaiwa kumbaka msichana mgonjwa alisema kuna hatua zinaendelea na kwamba hawezi kuzisema ni hatua gani kwa sasa. Naye Katibu tawala mkoa wa Tabora, Msalika Makungu aliwataka watumishi wa sekta ya afya kutambua dhamana waliyo nayo katika kuwahudumia wananchi na kuwataka kuwa mfano mzuri kwa jamii.

Chanzo: Mwananchi


 
Pole kwa mgonjwa alifanyiwa unyama, ila naona jamaa uvumilivu ulimshinda igunga kuna watoto wazuri balaa!!
 

Msichana alikuwa mgonjwa au mama yake ndiye alikuwa mgonjwa? Hizi habari umiza kichwa
 
Dunia ya sasa unabaka? Utakuwa una ugonwa wa akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…