Curtis De Mi Amor

Senior Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
136
Reaction score
514
Ukiiangalia Tabora kwanzia igunga , nzega, uyui, tabora sikonge, urambo, kaliua, utagundua huu mji ni wa kipekee sana.

Unaongoza kwa uzalishaji wa asali Tanzania nzima, unaongoza kwa uzalishaji wa karanga, unaongoza kwa uzalishaji wa maembe, unaongoza kwa uzalishaji wa ngozi, unaongoza kwa kilimo cha tumbaku na ndio mkoa mkubwa kuliko yote Tanzania. Historia ya huu mkoa ni mpana sana katika kukuza na kuendeleza ustawi na tamaduni za nchi yetu. Tabora ni mkoa wenye shule kongwe sana hapa nchini ikiwemo Tabora boys na girls na mirambo. Geographical yake kijani iliyochanganyikana na kichanga na udongo. Rutuba ya ardhi ni kichocheo kikubwa cha uchumi kwa wakazi wake.

Ni mkoa ambao umepakana na katavi, kigoma, shinyanga, singida na mbeya. Makabila makuu huko ni tabora ni wanyamwezi na wasukuma. Tangu enzi za ukoloni Tabora ndio ilikuwa ngome ya wajerumani na waarabu katika biashara. Wakati wa ujerumani ngome yao ilikuwa ni Tabora na walifanya biashara na machief wengi akiwemo chief mirambo! Huu mkoa una historia sana kuliko mkoa mwingine wowote ule Tanzania kwani hapa walitoka watu maarufu kama chief mirambo, chief isike, chief nyungu ya mawe n.k.

Hapa ndipo baba wa taifa aliposomea pale Tabora boys, ndipo alipotoka the late Samwel sitta, ndipo alipotokea prof. Ibrahim lipumba na wengineo wengi. Vuguvugu la kisiasa na ukombozi wa nchi ulianzia Tabora na ulimalizikia Tabora. Wajerumani wanaaminika kuacha mali zao nyingi sana za thamani katika mjinwa Tabora. Tabora kuna utajiri wa almasi na dhahabu na pia ikiwemo gesi asilia.

Kuna mapori na vivutio vingi vya wanyama! Na ndipo miti ya mininga ambayo ipo hatarini kupotea inapopatikana kwa wingi. Tabora ndio mkoa wenye hoteli kongwe kuliko zote nchini ambayo imehifadhiwa na inamilikiwa na shirika la reli. Tabora ni muhimu sana katika taifa letu kwani ni mkoa wenye mali nyingi, historia nyingi na vivutio vingi!

Tuendelee kuutunza huu mkoa, kuujali, kuuthamini na kuupa hadhi yake inayostahili kwa maana wote tunafahamu haswa namna Tabora ilivyojenga taifa letu la Tanzania.
 
Kwenye mkutano huu ndio Julius Nyerere alihutubia nakusema "..... Waingereza wasipotaka kutupa uhuru wetu basi tutawashitaki kwa Umoja wa Mataifa UNO, na UNO wasipochukua hatua basi tutawashitaki kwa Mungu..... "

Baada ya kusema maneno haya kwa uchungu mkubwa Julius alishindwa kujizuia na kulia hadharani na kufanya mkutano usismame kwa muda.


Huyu ndio Julius Nyerere baba wa Taifa na Mzalendo namba moja,Mzalendo halisi.
 
Hivi vibaka wamepungua huko Tabora? Maeneo ya isevya, ipuli na ng'ambo. Ila mademu wa kinyamwezi wanapenda sana chini. Bora usimoe hela ila uichakate mbususu!
 
Mwaga picha maneno matupu hayasaidii
 
Tabora kuna changamoto sana za ndoa za utotoni, nilishuhudia mabinti kibao wakiwa na watoto huko Kaliua, wengine wakiwa wameolewa kabisaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…