Tabora timu yao Iko vitani wao wanamshangilia adui uwanja mzima wamevaa nyekundu, nani awaambie Tabora ikishuka Simba hawataiona tena

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Somo la uzalendo limekuwa gumu sana hapa kwetu ,wenzetu huko epl na ulaya yote kwa ujumla timu ya nyumbani inapocheza hata na timu kubwa unayoishabikia uzalendo ni kuvaa jezi ya timu ya nyumbani ,skafu za timu ya nyumbani kuishangilia timu yenu ! Hakuna faida yoyote wakayooipata tabora ikiwa simba itashinda Leo ! Lakini pia tabora ikishuka daraja wasahau kuhusu kuziona simba au yanga hapo kwao ! Tujifunze uzalendo timu ya mkoa wako inapokuwa uwanjano onyesha mshikamano
 
Una kadi ya uanachama ya Tabora United? Unalipa ada stahiki?
 
Watu wa mikoani huwa washamba sana hapo wanaona wajanja kushabikia timu za Dar
 
AFYA YA AKILI MZEE.

HAPO NDIO UJUE AKILI ZA WATANZANIA
 
Mpira hauna unafiki kabisa, Bora mahusiano unaweza kujifanya unapenda ila kumbe hupendi bali football Haina hiyo, ukiwekewa msingi Fulani kwenye industry ya mpira na ukakua nayo basi ni ngumu kuacha.
 
Kama ishu ni uzalendo bado Tabora atakuwa na mechi na Yanga uwanja wao wa nyumbani,wazalendo tutakwepo
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…