Kuna tozo zinazodaiwa kuwa ni za usafi wa mazingira, ambapo kiwango cha malipo kinatofautiana kulingana na aina ya biashara. Hata hivyo, wanaokusanya tozo hizi hudai ni kwa ajili ya usafi wa mazingira na huduma ya ukusanyaji wa taka kwa kutumia magari ya manispaa, ilhali huduma hizo hazitolewi katika maeneo yetu.
Tunapowauliza, tunaambiwa huduma hizo zinatolewa katikati ya mji, stendi na sokoni pekee. Kama ni hivyo, sisi tunaofanyia shughuli zetu maeneo ya Lembeni tunatozwa kwa huduma ipi? Mara nyingi tunalazimika kuwalipa wazoa taka binafsi shilingi 500 ili wabebe taka zetu, halafu mwisho wa mwezi Manispaa inakuja tena kukusanya tozo za usafi. Hili linaonekana kuwa ni kutozwa mara mbili kwa huduma ambayo hatupati.
Jambo lingine linaloshangaza ni viwango vya tozo. Mfanyabiashara mwenye duka analipa Shilingi 10,000, wakati wakala wa huduma za fedha analipa Shilingi 15,000. Je, ni kwa msingi gani wakala wa fedha anatozwa zaidi, ilhali shughuli yake haitoi taka nyingi au kuchafua mazingira zaidi kuliko duka la kawaida?
Viongozi wa Manispaa ya Tabora, tunaamini zipo njia nyingi za kuongeza mapato ya halmashauri bila kuwaonea wafanyabiashara kwa kuwatoza huduma ambazo hawazipati. Tunaomba suala hili lipitiwe upya kwa haki na usawa.