Tabora: Utingo adaiwa kumuua dereva wake

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Benedicto Modest Mangi aliyekuwa dereva bajaji ya mizigo, Mkazi wa Mtaa wa Usule, Kata ya Mbugani Manispaa ya Tabora ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kisha mwili wake kufukiwa kwenye shimo tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi linalodaiwa kufanywa na mtu mmoja ambaye ni utingo wake waliyekuwa wakifanyakazi pamoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amethibitisha tukio hilo na kuwaeleza waandishi wa habari kwamba mtuhumiwa ambaye jina lake linahifadhiwa anadaiwa kufanya mauaji hayo kufuatia kumtuhumu dereva wake wa bajaji kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.

Kamanda Abwao amesema Utingo huyo ambaye yupo mikononi mwa Jeshi la Polisi akihusishwa na mauaji hayo inadaiwa aliwahi kumuonya dereva wake kwa kumtaka aachane na tabia hiyo kabla ya kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya mauaji hayo walipokuwa wanakwenda kijijini kubeba mzigo.

Inadaiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo utingo huyo alichimba shimo kisha kuufukia mwili wa dereva wake na kutokomea siku moja kabla ya Polisi kufanikiwa kubaini tukio hilo na kumkamata mtuhumiwa.

Chanzo: Azam TV
 
InShot_20230419_103116798.jpg
 
Picha hazifunguki,
habari yako haijakamilika mkuu
 
Ili iweje minyama unayokulaga haikutoshi acha ulafi na uroho!

Mkuu hiyo nyama inatosha Kama Kuna mtu hajashiba amalizie yeye
Umeanza kiherehere sasa😆
Haijanitosha ndio maana nataka manyama
Kama unayo jazia hapa
 
Umeanza kiherehere sasa😆
Haijanitosha ndio maana nataka manyama
Kama unayo jazia hapa
Nawe kafanye fumanizi ili utulutee unyama mtu gani wewe hushibi..? Habari imetosheleza kabisa ukipewa huo unyama utaomba na uwali maharage..! Acheni urafi
 
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Benedicto Modest Mangi aliyekuwa dereva bajaji ya mizigo, Mkazi wa Mtaa wa Usule, Kata ya Mbugani Manispaa ya Tabora ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kisha mwili wake kufukiwa kwenye shimo tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi linalodaiwa kufanywa na mtu mmoja ambaye ni utingo wake waliyekuwa
Dah!
 
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Benedicto Modest Mangi aliyekuwa dereva bajaji ya mizigo, Mkazi wa Mtaa wa Usule, Kata ya Mbugani Manispaa ya Tabora ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kisha mwili wake kufukiwa kwenye shimo tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi linalodaiwa kufanywa na mtu mmoja ambaye ni utingo wake waliyekuwa wakifanyakazi pamoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amethibitisha tukio hilo na kuwaeleza waandishi wa habari kwamba mtuhumiwa ambaye jina lake linahifadhiwa anadaiwa kufanya mauaji hayo kufuatia kumtuhumu dereva wake wa bajaji kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe.

Kamanda Abwao amesema Utingo huyo ambaye yupo mikononi mwa Jeshi la Polisi akihusishwa na mauaji hayo inadaiwa aliwahi kumuonya dereva wake kwa kumtaka aachane na tabia hiyo kabla ya kujichukulia sheria mkononi kwa kufanya mauaji hayo walipokuwa wanakwenda kijijini kubeba mzigo.

Inadaiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo utingo huyo alichimba shimo kisha kuufukia mwili wa dereva wake na kutokomea siku moja kabla ya Polisi kufanikiwa kubaini tukio hilo na kumkamata mtuhumiwa.

Chanzo: Azam TV
Kabla hujapigana na mwanaume mwenzio kwasababu ya mwanamke, mrekebishe mkeo kwanza..
 
Pole kwa wafiwa ,ndugu ,jamaa na marafiki na mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi
 
Back
Top Bottom