Siku chache baada Mwanachama wa JamiiForums.com kuandika juu ya hali ilivyokuwa katika Shule ya Msingi Nsololo kuhusu kuezuliwa kwa paa katika moja ya majengo ambapo hali hiyo ya jengo kutokuwa na paa kudai ilidumu kwa zaidi ya miezi miwili na nusu bila hatua zozote za kurejesha hali yake ya awali, hatua zimeanza kuchukuliwa.
Ujenzi wa maboresho ya jengo hilo umekuwa ukiendelea kwa siku kadhaa.
Ikumbukwe Februari 28, 2025, Mwanachama aliyeripoti taarifa hiyo alidai baadhi ya Walimu wamekuwa wakilazimika kukaa chini ya Mti ili kusubiri kuingia madarasani na kusababisha mazingira yasiyo rafiki ya utendaji kazi katika shule hiyo.
Jitihada za JamiiForums kumtafuta Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Uyui, Leokadia G. Humera kuzungumzia suala hilo, zinaendelea.