Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Igunga kuwachukulia hatua za haraka wakulima wote wa pamba ambao wamekataa kung’oa miti ya pamba ya msimu uliopita.
Wakulima hao wamekaidi kufanya hivyo kwa madai ya kutaka kulipwa fedha zao za mauzo ya pamba.
aidha, kwa upande wake Mkuu wa Mkoa alisema kampuni za ununuzi wa pamba kuchelewa kuwalipa fedha zao hakuwezi kuwa sababu ya wao kuvunja sheria na kanuni zinazosimamia zao la pamba.
Mwanri alitoa kauli hiyo jana wilayani Igunga wakati wa ziara yake ya kuhamasisha kilimo cha pamba na kukuta baadhi ya mashamba kando kando ya barabara yakiwa na mabaki ya miti ya pamba ya msimu uliopita ikiwa imeanza kuchipua upya.
Alifafanua kuwa baadhi ya wakulima wamekata miti ya pamba bila kung’oa na wengine hawakung’oa wala kukata na kuifanya ianze kuchipua baada ya mvua kunyesha, kitendo ambacho ni uvunjivu wa sheria ya pamba na kanuni zake.
Aliongeza kuwa kibaya zaidi wengine wameanza kupalilia mabaki ya miti ya msimu uliopita iliyochipua, kitendo kinachoonyesha kuwa wanataka kuiacha ili ionekane kama pamba mpya.
Mwanri alisema vitendo hivyo ni hatari kwa maendeleo ya zao hilo kwa kuwa vinaweza kusababisha wadudu na magonjwa ya pamba ya msimu uliopita kuhamia katika pamba inayopandwa hivi sasa.
Aliwataka viongozi kuanzia ngazi ya wilaya hadi kitongoji katika Wilaya ya Igunga kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa mashamba yote ili kuhakikisha wanaondoa mabaki ya pamba iliyopita.
Aidha, Mwanri alisema atarudi mara nyingine kuhakikisha kama hatua zimechukuliwa na kama akikuta hali ni kama ilivyo hivi sasa atalazimika kumchukulia kumsimamisha kazi kiongozi wa eneo husika na kuchukuliwa hatua mbalimbali za kisheria mkulima.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo, alisema wakulima wa pamba wa maeneo yote ambayo hawajalipwa fedha za pamba ya msimu uliopita wataanza kulipwa fedha zao.
Aliwataka kutumia fedha watakazozipata kwa ajili ya shughuli za maendeleo ikiwamo kufanya maandalizi ya kuwapeleka shule watoto wao na kuboresha kilimo cha pamba na mazao mengine.
Chanzo: Nipashe