Tabora: Watu tisa washikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuozesha binti wa miaka 13

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limewakamata watu tisa kwa tuhuma za kumwozesha binti mwenye umri wa miaka 13, Faudhia Mwinyi, mkazi wa Kazaroho, Kata ya Mbugani, kwa mwanaume Issa Ndambile (24), mkazi wa Geita. Ndoa hiyo ilikuwa ikifungishwa katika Msikiti wa Kazaroho, Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao, ameeleza kuwa binti huyo alihitimu elimu ya msingi mwaka 2023 na alichaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari mwaka 2024. Hata hivyo, mzazi wake alimzuia kuendelea na masomo na badala yake alichukua uamuzi wa kumuozesha.

Katika juhudi za kufuatilia suala hilo, Jambo TV imemtafuta Shekhe wa Mkoa wa Tabora, Ibrahim Mavumbi, ambaye amesisitiza kuwa kufungisha ndoa ya binti aliye chini ya miaka 18 ni kinyume cha sheria za nchi na pia ni kosa kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya Kiislamu.

Shekhe Mavumbi ameonya kuwa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Tabora halitasita kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa viongozi wa dini watakaokiuka sheria na kuruhusu ndoa za watoto.

Kuna watu wana asili ya akili ndogo tu, ni ndogo tu.
 
Back
Top Bottom