Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
MKOA wa Tabora umerudisha hazina Sh 326,192,517 walizopaswa kulipwa walimu wa Shule za Msingi baada ya kubainika kiasi hicho cha fedha kilizidi ikilinganishwa na madai yao halali. Madai ya walimu hao yalikuwa Sh 1,167,856,406 lakini baada ya kuhakikiwa yalionekana halali kulipwa ni Sh 841,662,889 hivyo fedha zilizobaki zimerudishwa hazina.
My take
Tukio hili ni kuonyesha uaminifu au kujipendekeza,
au wameogopa PCCB wangezifisadi wangejulikana,
au mgao haukueleweka mtu akamwaga unga,
Kama wamezirudisha hazina ina maana Tabora hakuna madai zaidi ya malimbikizo ya mishahara ya walimu
Nani alizidisha madai hayo na je kaadhibiwa?
Je hazina imeridhika kurudishiwa? kama wameridhika kabla ya kuzitoa ilijiridhisha kuwa hakukuwa na udanganyifu wa madai?
Mimi huwa najiuliza kwani tunapozungumzia utawala bora ni nini hasa ni kuona mtu anahubiri utawala bora au kuona matendo, je matukio kama haya yanahusika au hayahusiki na utawala bora elewa huu ni mkoa mmoja tu ambao angalau wamediliki.
Mwisho napenda kuuliza hapa mzembe ni nani aliyepeleka hazina idadi zaidi ya mahitaji au hazina iliyotoa pesa bila kuhakiki.
Ni tukio moja tu lakini tukijibu maswali hapo juu itawakilisha jinsi mali ya umma inavyotumika bila uangalifu, na ukiangalia kwa juu juu utasema kuna tatizo gani wakati pesa imerudi ilikotoka?