Tabora: Zahanati yazinduliwa katika Kijiji cha Kalangale

Tabora: Zahanati yazinduliwa katika Kijiji cha Kalangale

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wananchi wa Kijiji cha Kalangale, Kata Miswaki, Wilaya Uyui Mkoa wa Tabora wamenifaika na Mradi wa Zahanati uliokamilika na kuzinduliwa Mei 25, 2024.

Awali, walikuwa wakiangaika kufuata Huduma za Afya kwa umbali mrefu jambo ambalo ilikuwa ni tatizo hasa kwa akina mama Wajawazito na Watoto.

Mbunge wa Jimbo la Igalula, Venant Daud Protas ameshiriki uzinduzi huo ambayo ilianzishwa kwa nguvu za Wananchi pamoja na Mbunge kisha Rais Samia Hassan Suluhu akawapatia Shilingi milioni 50 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Mbunge huyo ameeleza kuwa baada ya kukamilika mradi Rais Samia ameongeza Shilingi milioni 25 kwa ajili ya vifaa tiba kwa niaba ya Wananchi.

Amesema awali Wananchi wa eneo hilo walilazimika Kwenda umbali wa umbali wa Kilometa 21.
WhatsApp Image 2024-05-26 at 20.07.21_64fdf93a.jpg

WhatsApp Image 2024-05-26 at 20.07.27_303de694.jpg

WhatsApp Image 2024-05-26 at 20.07.21_a7f0f8b8.jpg
Aidha, Mbunge kupitia ofisi yake wamezindua zoezi la ‘kumtua mama ndoo kichwani’ kwa kuzindua kisima cha maji kinachotumia pampu kijijini hapo.

Amesema tayari bomba hilo limeanza kuhudumia Wananchi hao wakiwemo jamii ya wafugaji na wakulima.
WhatsApp Image 2024-05-26 at 21.00.41_cf577e7d.jpg
 
Back
Top Bottom