Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), Japhet Justine amesema benki hiyo imejipanga kuhakikisha uzalishaji wa maziwa unaongezeka hapa nchini ili kutoa fursa kwa wazalishaji wadogo kuchangia ukuaji wa sekta hiyo. Justine amesema hayo wakati akizungumza na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) Prof. Philemon Wambura na kuongeza kuwa, shughuli za usindikaji wa maziwa zipo chini ya kiwango kutokana na uzalishaji duni wa maziwa, hali ambayo amedai inarudisha nyuma ukuaji.SOMA ZAIDI.
TADB kuhamasisha uzalishaji maziwa