Tafadhali anayeuelewa Utangazaji wa Samuel Nathaniel Sasali wa Clouds 360 anieleweshe

Tafadhali anayeuelewa Utangazaji wa Samuel Nathaniel Sasali wa Clouds 360 anieleweshe

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Moja wapo ya Kanuni za Utangazaji hasa wa Runinga ni Mtangazaji Kuuvaa Uhusika hasa wa Jambo fulani unalolitangaza ili Hadhira nayo ikuelewe.

Tuko katika Kipindi cha Majonzi cha Kushangaza Mtangazaji huyu Samuel Nathaniel Sasali wa Clouds 360 hayupo Kimsiba Msiba na Yeye muda wote tu ni Kufanya Mizaha isiyo ya lazima huku akidhani anapatia wakati kumbe ndiyo anaharibu zaidi.

Na sijui hii style ya Kutangaza kwa Kuongea haraka haraka huku akiwa anahema kama vile anakimbizwa na Mbwa Mwitu ameitoa wapi.

Enyi Clouds Tv jitahidini sana Kuiga jinsi ya Utangazaji wa Live Coverages kutoka katika Media kama za Citizen Tv ( Kenya), ITV Tanzania) na hata TBC1 (Tanzania) na mkiweza tafuteni Mtangazaji anayeendana na hili na siyo kama afanyavyo huyu Sam Sasali tafadhali.

Mwisho nimeangalia Utangazaji wa karibia Tv Local Channels zote nimeona karibia nyingi Kipindi hiki cha Maombolezo hazifanyi Mizaha na hata Nyuso tu za Watangazaji wao zinajielezea, ila kwa Clouds Tv naona Mizaha Mizaha ni Mingi, Upuuzi nyakati fulani na Utoto kwa baadhi ya Watangazaji wao.

Najua hapa JF kuna Wabobezi wa Masuala ya Habari, Utangazaji na Mawasiliano hivyo naamini mtanisaidia Kujua aina hii ya Utangazaji wa huyu Samuel Nathaniel Sasali wa Clouds 360 hasa katika ( Live Coverages ) na Utangazaji wa Kiujumla wa Clouds Tv hasa katika Kipindi hiki cha Majonzi ya Kumpoteza aliyekuwa Rais wetu Mpendwa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
 
Ila kuna mambo yanafurahisha sana, jana kuna mwamba alikua anahojiwa clouds Tv, na nukuu "katika kipindi cha rais magufuli ata mishahara tunapokea kwa wakati yani tarehe 21-25 tayari umepata mshahara, tofauti na vipindi vya nyuma ambapo tulikua tusubiria mpaka tarehe 32, 31 si unkumbuka" ..
 
Ulitaka atangaze akiwa analia au?

Wapishe JF Intelligent Members waje Kuujadili huu Uzi na Wewe nakuomba kaa pembeni uone Madini yao ili Basi huo Upumbavu unaokutawala Ubongoni mwako na Uliorithishwa ama upungue au ukutoke kabisa sawa?
 
Ila kuna mambo yanafurahisha sana, jana kuna mwamba alikua anahojiwa clouds Tv, na nukuu "katika kipindi cha rais magufuli ata mishahara tunapokea kwa wakati yani tarehe 21-25 tayari umepata mshahara, tofauti na vipindi vya nyuma ambapo tulikua tusubiria mpaka tarehe 32, 31 si unkumbuka" ..
huyo mwamba alitisha sana kama astra zeneca
 
Back
Top Bottom