Pamoja na Clouds Media (media category) kutokuwa kituo cha habari ila cha burudani kuna wakati wanajisahau sana tena sana.
Niliwahi kuandika sehemu, mojawapo ya usajili wa chombo cha habari hapa nchini unaendana na category unayopewa/omba Kulingana na hitaji lako au eneo unalotaka kuwekeza chombo chako.
Ukija upande wa hao jamaa, wao walikuja kama kituo cha burudani kwa sana na tokea mwanzo ukipiga picha utagundua walijazwa au kuajiliwa waongeaje wenye maneno mengi, utani nk haikuwa taaluma.
Hiyo imeendelea pale ndani kiasi kwamba hata kukiwa na jambo/habari ngumu wao wanaiweka kiburudani, ucheshi, utani nk ili kufikia hadhima ya usajili wao.
Kuna baadhi ya watangazaji wapo kikazi na wengine baada ya kuingia darasani ndiposa utawasikia 'wanajinasibu' kupitia mic "kama mwalimu alivyotufundisha" au utasikia "juzi class tuli tulipewa assignment flani"
👉🏾Tumsamehe tu huyo jamaa maana hajui alitendalo.