Tafadhali anayeuelewa Utangazaji wa Samuel Nathaniel Sasali wa Clouds 360 anieleweshe

Hili tatizo la interruptions za watangazaji siyo kwa hao wa clouds redio peke yao ni ktk tasnia nzima hapa bongo wana kasumba hiyo.

Hata miziki ikiwekwa inakatizwakatizwa hovyo.

Miziki mingine hunoga mwishoni zaidi wao wanakatiza! [emoji57][emoji57]

Au wanajidai kurudia mashairi ya kwenye miziki Yani inaboa jamani ! [emoji57][emoji57]
 
Watangazaji wa bongo wanatakiwa wawe na listening skills za kutosha hususa wanapokuwa kwenye vipindi vya mahojiano, presentations n.k

Kama ni ku interrupt muwasilishaji inatakiwa mara chache tena pale panapostahili kwa niaba ya msikilizaji/mtazamaji.

Mfano kile kipindi cha ITV cha dakika 45 n.k

Yani unakuta mwasilishaji wa mada anaongea jambo muhimu anakuwa interrupted unnecessarily kisha anasahau points za msingi alizokusudia kuziwasilisha.

Watangazaji and the like mnapaswa kujifunza zaidi.

Tukirudi kwenye jinsi ya kuhoji huko ndo kabisa wengi hawajui namna nzuri ya kuuliza maswali muhimu kwa niaba ya msikilizaji na mtazamaji.

Mwingine kaja na fix na hadaa zake anaachwa aseme mpaka mwisho bila kumheld responsible kwa kumbana kwenye maswali yenye hoja.
 
Live your life mkuu, mambo mengine yatakupotezea muda. Kwa nini unaweka kichwani mambo ambayo hayana msingi na hayana nafasi ya kujadiliwa humu. Next time njoo na facts na sio kujadili watu, kwa maana small minds discuss people.
 
Sasali anamhubiri Yesu zaidi ndiyo maana huwezi muelewa.
Mungu ambariki sana.
 
Duh kwani watu wanaomboleza kwa kufanana ?, Ingawa simjui jamaa ila watu wapo tofauti..., mfano wajaluo wao wanaomboleza kwa kucheza mziki..., by the way ndio maana kuna choice hao wakikuboa tune channel nyingine sasa ukitaka wote wawe serious wapenda mzaha wataangalia nini?
 
Mwacheni Doctor bingwa wakusoma Magazeti Tanzania nzima,,Me namkubali sana mchungaji Sasali,,Yule ni MC wa masherehe,,Fun guy nahisi hii imemuathiri
 
Kwa nijuavyo mimi Sasali ni mlokole... kuna ile imani kila mtu anayo. Sam is different katika uombolezaji wake. Na usifikiri Sam hajaguswa. Usilolijua ni kama usiku wa kiza. Sam amekula sana maisha Awamu hii. Si lazima kila mtu aonyeshe hadharani namna ameumizwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…