Tafadhali Anne Makinda jihadhari kwani Pius Msekwa si saizi yako. Msekwa katumia usomi kusema akina Halima Mdee wamefutwa Ubunge

Hawa viongozi wastaafu wanatakiwa kuacha kiherehere, wakae kimya kwa sababu ulimwengu wa sasa kila mtu anajua vitu vingi.
Kuwataka wakae kimya wasitoe maoni ni udikteta na kuminya uhuru wa watu kutoa maoni.

Kwani tukiwakosoa kwa staha kuna ubaya gani?
 

wenzenu huwa tunaiona akili mbovu ya mtu katka sentesi zake mbili au tatu za mwanzo.

kitendo cha kukataa mama makinda kushauri vyombo vya habari,tayari lilikuwa ni tatizo.
hawa wazee wamekuwa wakisifiwa sana wanapotoa kauli kama hizi na kuonekana mashujaa,kinyume chake huwa wanaonekana ni wazee waliochoka kufikiri,wanapalilia njia za watoto wao nk.

sasa subiri siku azungumze tofauti,huyu huyu atakuwa wa kwanza kutamka mzee akae kimya.
 
Kisha wenyewe wanadai uhuru wa kutoa maoni!!
 
Mh! Hii kali kweli kweli, amekufanya nini huyu mama mpaka unampiga spana nzito namna hii bila huruma?
Kwakuwa huyu Mama kachagua kukaa kimya bila kuandika chochote. Hivyo Historia haimkumbuki. Tatizo lake ni pale anapolazimisha Historia kutowakumbuka wenye Historia ktk Nchi hii. Sasa acha apigwe spana akili zimkae sawa.
 
Mh! Hii kali kweli kweli, amekufanya nini huyu mama mpaka unampiga spana nzito namna hii bila huruma?
Hawaihitaji huruma hawa waharibifu wa nchi hii!Atasemaje waandishi wamuache wakati ndiyo muda sahihi wa mzee kugawa urithi wake kimawazo kwa vijana wa taifa hili?
 
Makinda anategemea apewe teuzi.
Msekwa haelewi na hataki huo upuuzi
 
Huko sahihi na Ndugai aache kuinajisi katiba kwa kuwalinda kinyume na katiba na sheria, maana wakishauriana na jiwe utaona matokeo yake!
Mimi nazungumzia hii tabia ya kumsifia mtu pale anaposema jambo lenye kufurahisha watu fulani ila siku akiongea lisilo furahisha humtoa akili mtu huyo.
 
Hawezi kuja kajiaibisha mwenyewe na mihemiko yake juzi hapa ya vi uzi uzi kuponda cdm juzi baada ya tamko la kamati kuu kuwatimua yeye mwenyewe kajificha.
Amekuja. Ame-react.

Bila shaka atapandisha uzi ku-support, ku-oppose ama kuwa-neutral tu dhidi ya Hoja za mdogo wenu.
 
Mimi nafikiri kwa akili iliyosahihi, ikitokea Mzee Msekwa, mtu au kiongozi yeyote yule akatoa mawazo yake kwenye Jambo lolote ambalo linathibitika kuwa kinyume na ushauri aliotoa, kumkosoa ni halali, lakini kwa hili la wabunge was chadema Mzee Msekwa ameongea kwa reference ya katiba Kama ilivyo Sasa, utamkosoa kwa kutumia reference ipi?
 
Mimi nazungumzia hii tabia ya kumsifia mtu pale anaposema jambo lenye kufurahisha watu fulani ila siku akiongea lisilo furahisha humtoa akili mtu huyo.
Kunatofauti Kati ya kufurahisha na kuongea kitu sahihi.
 
Hana uwezo hata wa kulegeza gidamu za viatu vya Msekwa huyu mama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…