Tafadhali Ewe Mwanaume uliyemtesa Mtangazaji wa Magic fm Mary Edward mwombe radhi utuokoe Wanaume wote!

Tafadhali Ewe Mwanaume uliyemtesa Mtangazaji wa Magic fm Mary Edward mwombe radhi utuokoe Wanaume wote!

Mwambieni Kibwana Dachi a.k.a google amshauri.Au Pascal Mayalla alishawahi kuwa mfanyakazi pale AMG apeleke ujumbe huu.
 
Nadhani ni vyema mzazi wa kiume kazi yake iwe kumpa mtoto wake wa kike kiasi fulani cha pesa. Maana kila mwezi anakua na mahitaji hayo.

Ni kweli ni watoto zetu, lakini wanahitaji privacy.
Hao ni wake wa baadae wa vijana wa wazee wengine.

Angesema kumnunulia mpenzi sawa ila dota nope!
 
Acha Bange / Bangi tafadhali sawa? Mimi mademu zangu wote huwa namalizana nao pale pale kama Kondakta na Abiria ndani ya Daladala sasa leo unavyoniambia kuna Demu sijui nilimkosea na sijamwomba Msamaha nashindwa Kukuelewa! Niliacha kupenda rasmi, kuwanyenyekea hawa Viumbe na Kuwabembeleza kama Mwendawazimu mwaka 2010 na sasa hivi ukinikuta namwambia Demu ' Nakupenda ' jua namjaza tu Upepo / namtengeneza anipanulie ' Kitufe ' chake Mwanamume nipite zangu na nionyeshe ' Urijali ' wangu uliotukuka Kwake kisha ndiyo ' ntolee ' hiyo.
Kumbe na wewe una shida mahali fulani...mwanamke alokutenda akuombe msamaha ili yaishe uanze kuwapenda wanawake wako
 
Ni Mtangazaji ambaye ukiwa unamsikiliza akitangaza au hata akiwa anachangia mada fulani katika Kipindi chao cha asubuhi hutopata shida sana kujua ya kwamba lazima tu alikuwa na Mahusiano mabaya huko nyuma na Mtu wake na alimtenda vibaya mno ndiyo maana huwa anakuwa ' very emotional ' kwa mambo ya Kimahusiano yanayowahusu Wanaume.

Mary Edward Mzurikwao hajawahi kuwa ' neutral ' katika ' udadavuaji ' wake wa masuala ya Kijinsia au Mahusiano na kuna muda utaona kabisa kwamba tukio fulani limemtokea Mwanamke mwenzake kwa Kosa lake mwenyewe lakini bado utamsikia Mtangazaji huyu akiendelea kuwaponda / kuwananga / kuwasema Wanaume utadhani labda Mimba iliyomleta Yeye hapa duniani haikutokana na juhudi za huyo huyo Mwanaume ambaye leo anamchukia.

Mtangazaji Mary Edward amekuwa na tabia za kulazimisha mambo ambayo hata Kidini tu na Kimaadili ya Kiafrika hayawezekani kiasi kwamba huwa namtafakari na simpatii majibu sana sana huwa naona ananikera tu.

Kwa mfano leo asubuhi amekazania kabisa kusema tena kwa amri kabisa akitutaka Wanaume wote kuwa na tabia za kuwauliza Mabinti zetu kama wapo katika Siku zao za Hedhi ( Menstrual Period / Cycle ) na kisha tuwe tunaenda kuwanunulia Madukani na kuwapa ili wazitumie na kwamba ikiwezekana tuwe pia tunawauliza kama wamemaliza Siku zao na kuwafundisha jinsi ya Kuoga ili ' Kujiswafi ' vizuri huko ' Ikuluni ' Kwao.

Hivi huyu Mtangazaji Mary Edward na Yeye Baba yake Mzazi alikuwa akimfanyia yote haya pale alipovunja Ungo? Halafu ni kwanini anapenda sana kuitumia Magic fm kama ' platform ' yake ya kuwasema vibaya Wanaume? Kama aliumizwa na kuudhiwa na Mahusiano yake na Mwanaume wake tafadhali watafutane kimya kimya na wayamalize lakini siyo kila uchao kujifanya anakuwa ' too emotional ' kwa ' issues ' za Wanaume.

Abadilike upesi tafadhali na naamini kwa ' Uzi ' wangu huu ' message sent and delivered ' na Kesho kama kawaida yangu nitakisikiliza Kipindi chao ili nione ' reaction ' yake juu ya huu ' Uzi ' hasa nikiamini kwamba karibia 99% ya Watangazaji wa hicho Kipindi ni wana JF wazuri tu na tunao humu 24/7 tukitiririka na kuserereka pamoja.

Nawasilisha.
Sitochangia hii mada hadi niione picha ya Mary Edward
 
Sitochangia hii mada hadi niione picha ya Mary Edward
Huyo
Screenshot_20180531-234751.jpg
 
Nikiikumbuka historia yake Binafsi tokea alipokuwa katika Kipindi Kigumu tokea huko Dodoma, kisha akawa anasaka nyoka ( namaanisha anatembea kwa kukatiza mitaa huku na kule kutafuta habari ), mara akinyanyasika na Mabosi zake katika Media ya huko Dodoma, halafu akapata msaada wa Mtu mmoja ( jina Kapuni ) hadi kuja Dar es Salaam kisha akaendelea zake za zoezi la ' Kusaka Nyoka ' hatimaye Njemba kadhaa zikambeba kwa makubaliano ' maalum ' ndipo akaanza kufanya Kazi hapo alipo ambapo pia mwanzoni alikuwa hakubaliki huku akipuuzwa na kudharaulika na aliowakuta kutokana na Elimu yake aliyokuwa nayo lakini bado alijikaza, kuvumilia na kupambana na hatimaye leo amefikia hapo alipo Kikazi / Kiutangazaji napata faraja sana na kuamini kuwa kumbe hapa duniani hakuna aliyezaliwa kuja ' Kunyanyasika ' na kwamba kila Mtu Mwenyezi Mungu ana makusudi nae makubwa tu hapa duniani hivyo hatupashwi kukata tamaa hata kidogo.

Sina Ubaya / Uadui nae tena hakuna Mtangazaji ambaye nilivutiwa kumfuatilia kama huyu Mary Edward Mzurikwao hasa baada ya Mtu mmoja ambaye anamjua in and out kunipa Historia yake ya Kimaisha, kote alikopitia, changamoto alizokutana nazo na mpaka hapo alipo sasa ila anapoharibu ni hapo tu Kupenda Kwake kuwa ' too emotional ' kwa masuala yanayowahusu Wanaume huku akidhani kwamba Wanawake hawakosei na hawana madhaifu yao.

Kama akibadilika na kuyafanyia Kazi haya mapungufu yake namtabiria mambo makubwa sana na ya Kimafanikio Dada na Mdogo wangu Mary Edward Mzurikwao kwani ana vitu vingi sana vizuri vya Kiutangazaji ambavyo Watangazaji wengine wengi wa Kike hawana na namkubali zaidi kwakuwa pia ni Mdada mwenye hofu sana na Mungu ( ni Mcha Mungu ) mzuri sana japo akiwa anaongea ' Kiredio ' unaweza ukadhani ni wale wale tuliowazoea katika Media zingine.
 
Acha Bange / Bangi tafadhali sawa? Mimi mademu zangu wote huwa namalizana nao pale pale kama Kondakta na Abiria ndani ya Daladala sasa leo unavyoniambia kuna Demu sijui nilimkosea na sijamwomba Msamaha nashindwa Kukuelewa! Niliacha kupenda rasmi, kuwanyenyekea hawa Viumbe na Kuwabembeleza kama Mwendawazimu mwaka 2010 na sasa hivi ukinikuta namwambia Demu ' Nakupenda ' jua namjaza tu Upepo / namtengeneza anipanulie ' Kitufe ' chake Mwanamume nipite zangu na nionyeshe ' Urijali ' wangu uliotukuka Kwake kisha ndiyo ' ntolee ' hiyo.
GENTAMYCINE. Nadhani baada ya kuacha kupenda , sasa una waumiza wewe kwa style yako mpya.
Siwatetei , ila usichojua ni kwamba mwanamke huwekeza hisia kwako, unachofanya sasa hivi ni kuwavunja mioyo. Ndio hawa watangazaji wanaolalamika.

Kwann usifanye hiv, mwanamke anapokuja kwako umchane ukweli tu kuwa ww kupenda ni ngumu.. kwamba hautakaanae muda mrefu then ajue moja asepe kabla hujamuachia vidonda.

Instead of kuendelea kuongeza janga la wanawake wa aina hii . Tuounguze kwa kuanza kuwamakini na machaguo yetu wenyewe.
 
aisee GENTAMYCINE unaanzaje kumponda mtoto mzuri namna hii haijalishi ana mapungufu gani Hakuna mkamilifu duniani na amini nakuambia asilimia 90 ya watangazaji wanayoyaongea hayan ukweli huongea tu kufurahisha wasikilizaji
Sio kumponda ni kumwambia ukweli. Sasa kama mtu kutwa kulaumu wanaume, basi yeye anashida mahali.
Amlaumu huyo mwanaume wake aliyemuachia vidonda, na sio kulaumu wanaume wote. Maana si wanaume wote ni wabaya...
 
Radio Hizo sisikilizi! sijui kwanini?

Hivi mtu una Smartphone,unabundle,una Instagram,una facebook,una JAMII FORUM,una Whatsapp Bado unasikiliza Radio??? Kwanini labda?

Mada zote zinazo Jadiliwa kwenye Radio Jamii Forum zinakuwaga zilijadiriwa kitambo!!!!!

Hivi Radio kweli mm hapana Bado hujanishawishi kusikiliza Radio labda nikija kuwa Sina smartphone
 
Nikiikumbuka historia yake Binafsi tokea alipokuwa katika Kipindi Kigumu tokea huko Dodoma, kisha akawa anasaka nyoka ( namaanisha anatembea kwa kukatiza mitaa huku na kule kutafuta habari ), mara akinyanyasika na Mabosi zake katika Media ya huko Dodoma, halafu akapata msaada wa Mtu mmoja ( jina Kapuni ) hadi kuja Dar es Salaam kisha akaendelea zake za zoezi la ' Kusaka Nyoka ' hatimaye Njemba kadhaa zikambeba kwa makubaliano ' maalum ' ndipo akaanza kufanya Kazi hapo alipo ambapo pia mwanzoni alikuwa hakubaliki huku akipuuzwa na kudharaulika na aliowakuta kutokana na Elimu yake aliyokuwa nayo lakini bado alijikaza, kuvumilia na kupambana na hatimaye leo amefikia hapo alipo Kikazi / Kiutangazaji napata faraja sana na kuamini kuwa kumbe hapa duniani hakuna aliyezaliwa kuja ' Kunyanyasika ' na kwamba kila Mtu Mwenyezi Mungu ana makusudi nae makubwa tu hapa duniani hivyo hatupashwi kukata tamaa hata kidogo.

Sina Ubaya / Uadui nae tena hakuna Mtangazaji ambaye nilivutiwa kumfuatilia kama huyu Mary Edward Mzurikwao hasa baada ya Mtu mmoja ambaye anamjua in and out kunipa Historia yake ya Kimaisha, kote alikopitia, changamoto alizokutana nazo na mpaka hapo alipo sasa ila anapoharibu ni hapo tu Kupenda Kwake kuwa ' too emotional ' kwa masuala yanayowahusu Wanaume huku akidhani kwamba Wanawake hawakosei na hawana madhaifu yao.

Kama akibadilika na kuyafanyia Kazi haya mapungufu yake namtabiria mambo makubwa sana na ya Kimafanikio Dada na Mdogo wangu Mary Edward Mzurikwao kwani ana vitu vingi sana vizuri vya Kiutangazaji ambavyo Watangazaji wengine wengi wa Kike hawana na namkubali zaidi kwakuwa pia ni Mdada mwenye hofu sana na Mungu ( ni Mcha Mungu ) mzuri sana japo akiwa anaongea ' Kiredio ' unaweza ukadhani ni wale wale tuliowazoea katika Media zingine.
Mkuu huyu bint simjui sana ila najua pale paliponigusa, ushauri wangu kwake na kwa wengine wenye tabia kama yake wanapokuwa katika mahusiano wasijisahau sana wajue kuna leo na kuna kesho ambayo haifanani na jana pia kuna Muumba ambaye halinganishwi na chochote na maamuzi yake ni ya mwisho pia. Wasipende kujisahaulisha kwamba wamefika hapo ndipo wanapojikuta katika hali kama hiyo nadhani panatosha
 
Back
Top Bottom