Tafadhali jihadhari na tapeli huyu wa Instagram!

Tafadhali jihadhari na tapeli huyu wa Instagram!

Ukiona tu muuzaji amezuia comments kwenye page yake hiyo ni dalili mbaya namba moja kabla hata haujaenda mbali
Screenshot_20201214-155746.jpg
 
Kuna matapeli maarufu kwenye mtandao wa Instagram, hii account yenye jina la zanzibar_electronics_og ni matapeli ambao ukiangalia utadhani ni wafanyabiashara wakubwa kulingana na followers.

Lakini hawa ni matapeli ambao hawana duka physically na wala hawana bidhaa yoyote, wanawaibia watu kwa kuwaahidi wafanye malipo na kisha watawatumia bidhaa zao, wamekua wanabadilibadili jina la kampuni, walijifanya wapo Darajani, Zanzibar ila kesi zilivokuwa nyingi sasa wamebadili wanadai duka lao lipo Chakechake Pemba, angalizo hakuna duka la electronics hapo kwenye sehemu.

Tafadhali tusaidiane kuwaokoa ndugu zetu wasitapeliwe zaidi. Sambaza kwa wengine wengi. Ahsanteni sana.
Nilishawahi kuwauliza ni kwanini wanatumia picha za maduka ya Kariakoo na wao wapo Pemba!!!? Niliambulia matusi mazito!
 
ili kuwajua utakuta bidhaa moja kwenye page mbali mbali bei haitofautiani sana mfano 320,000 au 300,000 ila kuna page moja bidhaa ile ile anaiuza 200,000. ukiomba location ya duka utaambiwa sijui mbagala au kigamboni ukitaka maelekezo vizuri ufike hujibiwi. picha za insta nyingi zimekuwa cropped kuziba majina halisi ya wauzaji.
 
Hahaha hawa ni matapeli wa wazi wazi kabisa.... Juiz niliwapigia simu akapokea mdada mmoja nikamuuliza mbona mmelimit comment kwenye page yenu akasema okay watafungua

Nikamuuliza tena mbona ninyi mko pemba huko na wateja wenu wengi wako bara?... Mdada akaaanza kutoa matusi mazito mazito.

Picha zao nyingi wanazitoa jaden home store na maduka ya kariakoo
 
kuna wengine wanajiiita rashidi_electronics bei zao zinatia mashaka sana, alafu hawaruhusu comments
Hata hao waliowatapeli wanaolalamika hapa wamefunga comments. Na wale wanaoruhusu comments hawatoi majibu ya maswali wanayoulizwa.
Mie nimenunu bidhaa online, lkn nililipa walipoleta home (cash on delivery). Bidhaa ilikuwa mpya na bado naitumia mpaka leo. Ila hawa wanaosema lipa kabla, hell no my dear.
 
Back
Top Bottom