Tafadhali kwa mtu yeyote ambayo ameshakutana na tatizo kama hili kwnye papai

Mbogo_beichee

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2021
Posts
224
Reaction score
608
Habarini wana jamvi wote. Natumai wote tupo poa, tunajenga taifa. Naomba niende kwenye maada moja kwa moja.

Mimi ni mkulima wa mazao ya muda mrefu na mfupi. Sasa mwaka jana nilifanikiwa kulima zao la papai.

Kuanzia kufulia miche mpaka kupanda shambani nilifanikiwa kwa asimilia nyingi tuu. Sasa likaja tatizo wakati wa mvuno wa kwanza mapapai yalikuwa yakikomaa kuelekea kuiva yanatengeneza Vibarango vidogo vidogo kadili papai linavokuwa linakua, na mpaka papai likikomaa kabisa basi hivo vibarango vinakua vingi na kuwa vikubwa zaidi,

Pamoja na hilo shepu ya papai inabadilika kabisa inakua haieleweki. Tafadhali kwa mtu yeyote ambayo ameshakutana na tatizo kama hili, anipe ushauri wa jinsi alivotatua.

Papai zimepandwa mbegu aina ya Sinta F1, shamba lipo sehem ambayo ina baridi japo sio sana ila na joto sio kubwa sana.
Screenshot_20241012-121952_Gallery.jpg
 
Aisee huu ugonjwa sio wa hospitali huu
 
Mbolea na Maji ulizingatia maana mimi mipapai yangu haijawahi kuugua huo ugonjwa na yapo vizuri tu hapo kikubwa ni aina ya udongo usiwe ule udongo rahisi kushabuliwa na wadudu, mbolea iende na vipimo na maji yahusike hata kwa wiki mara 3, na mazingira unayoishi je hakuna uwezekano wa visababishi vya magonjwa ya mimea?
 
Baridi? usha tamka Baridi umemaliza kila kitu, Kabla hujalima zao angalia linahitaji hali ya heaa ya aina gani, Papai mfano halipatani kabisa na kitu kinaitwa baridi, na linataka jua la muda mrefu sana.

Tunaforce sana mazao
 
Vipi mipapai dume imo shambani? {hii ni kwa umbo la tunda}

kuhusu ugonjwa nenda kwa bwana kilimo na tunda hata moja waeneo lako atakupa njia sahihiya kukabiliana na hali hiyo
Hapana sio dume. Ni miche karibu yote ina tatizo hilo. Ngoja nitamtafuta bwana shamba
Mbolea na Maji ulizingatia maana mimi mipapai yangu haijawahi kuugua huo ugonjwa na yapo vizuri tu hapo kikubwa ni aina ya udongo usiwe ule udongo rahisi kushabuliwa na wadudu, mbolea iende na vipimo na maji yahusike hata kwa wiki mara 3, na mazingira unayoishi je hakuna uwezekano wa visababishi vya magonjwa ya mimea?
Mbolea iliwekwa na maji ilikua masika mvua ni nyingi tuu. Wengine wanasema ukungu wengine wadudu. Wewe unahudumiaje mkuu
 
Baridi? usha tamka Baridi umemaliza kila kitu, Kabla hujalima zao angalia linahitaji hali ya heaa ya aina gani, Papai mfano halipatani kabisa na kitu kinaitwa baridi, na linataka jua la muda mrefu sana.

Tunaforce sana mazao
Nimekusoma mkuu. Hapo kwa wazo lako nifanyaje kwenye msimu huu wa pili wa kuvuna?
 
Kwa uzoefu wangu, na uliposema baridi naona ni ugonjwa wa dark spot huo kama kutu.

Chukua dawa inaitwa FUNGOFORCE (mancozeb 64% + Metalaxyl 8%) upige shamba lako. Matumizi kwa kawaida ni 50g kwa lita 20 za maji. Mipapai haipatani na baridi. Ukipanda miche mpya ipige dawa ya kuzuia kutu (Z-Force) Mancozeb 80%.

Humo tu.
 
Hapana sio dume. Ni miche karibu yote ina tatizo hilo. Ngoja nitamtafuta bwana shamba

Mbolea iliwekwa na maji ilikua masika mvua ni nyingi tuu. Wengine wanasema ukungu wengine wadudu. Wewe unahudumiaje mkuu
Hujajibu swali langu nimekuuliza maeneo ya jirani hakuna kusababishi chochote cha magonjwa ya mimea? Jirani na shamba lako si unaelewa magonjwa ya mpapai yanapitia njia 2 ardhi au hewa kwa km ugonjwa hujapitia kwenye ardhi utapitia kwenye hewa mmea unayoipokea na hio ndio inaleta athari kwenye matunda ya mmea hio ipo hata ukilima mahindi mabichi au mapera au machungwa tena machungwa nje safi ndani sponchi hakuna maji hakuna radha matikiti the same parachichi the same ndizi ndio wamebuni busta ya kuziivisha zinakaangwa na kemikali ndizi mbichi zinaivishwa kwa kutumia kemikali kisha tunaletewa tule
 
Back
Top Bottom