Hujasikia sera za trump?,okay tuachane na trump,nitajie number ya wabongo ambao wakienda huko wanapata ''smart job'
"Smart job" zipo nyingi tu na wageni wa nchi mbali mbali wanazifanya.
Tatizo, Wabongo wasomi ni wachache. Mashirika makubwa ya Marekani kama Google au MIcrosoft na hata Serikali ya Marekani huwa wanatafuta watu katika Ivy League Universities kama Harvard na Princeton. Kazi za mishahara midogo Ndio wanawapa wahitimu wa vyuo vingine. Lakini bila MBA ya Harvard au Yale au vyuo vingine mashuhuri, hupati kazi kama CEO kirahisi. Ndio maana huwezi kukuta Mbongo CEO wa top 100 huko. Huko ni Wahindi , Warusi na Wayahudi tu.
Kazi za $50,000 kwa mwaka zipo lakini kwa Marekani ni hela mbuzi. Ukiwa na watoto 3, mikopo ya benki ya kununua nyumba, magari na kulipa madeni ya vyuo vikuu, huwezi kuweka akiba nyingi benki.
Wabongo wengi ni maneno mengi, action kidogo. Ukweli unauma lakini uwezo wa kusoma nje hatuna na elimu ya Tanzania haimtayarishi Mbongo kupewa wadhifa wa kazi za mishahara ya $1 million au wadhifa mkubwa kama wanavyopewa Ma CEO wa Kihindi hapo Google au Citibank.
Pia, hali ya kiuchumi ya maisha duniani inabadilika. Marekani ni military superpower sio tena Economic Superpower. Uchumi wake ni wa kukopa, raia wake wengi wanaishi kwa kukopa. Karibu kila Mmarekani anamiliki credit card zaidi ya nne. Watu wengi wanaishi "paycheck to paycheck". Wengi hawana uwezo wa kumwona daktari kwa kuwa hawana "insurance".
Raia wenye credit card wana deni la $900 bilioni mwaka 2016. Kama wana kazi nzuri na mshahara wa kutosha , wangeweza kulipa madeni yao kirahisi.
Wenye uwezo wa kulipa bili zao za credit card kwa mkupuo kila mwezi ni 35% tu. Wengi wanalipa pole pole, hawana uwezo.
Ndio maana watu wanaandamana na kutaka kula Keki kubwa zaidi ya Taifa. Uchumi wa Marekani umeshikiliwa na raia wachache. Na ulikuwa hivyo kwa miaka mingi tu. Ndio maana utasoma kuwa kuna maandamano ya " we are the 99%", wanataka kupewa tiba ya bei nafuu, kazi wanazoweza kulisha familia zao, na misaada ya kusoma kwa bei nafuu. Uchumi umeshikwa na wachache sana Marekani. Angalia Gini- coefficient ya Marekani , 80.5, the highest in developed world. Yaani, utajiri wa nchi umeshikwa na watu wachache, japokuwa Marekani ni nchi tajiri kuliko wote duniani.
Ndio maana nilimjibu Nyani kuwa Asia Kuna maisha mazuri zaidi kwa wananchi wao. China kuna "middle class" milioni 300, karibu sawa na raia wote wa Marekani. Thailand, Indonesia na Malaysia wananchi wenye uwezo wa Kati (middle class) wanaongezeka kila mwaka huku Marekani umeganda. Kila siku viwanda vinafunguliwa na kuzalisha Mali ya bei rahisi kuliko Marekani. Walmart peke yake inanunua asilimia 10 ya Mauzo ya nje ya China. Hii tu inakuonyesha jinsi gani wananchi wengi wa Marekani walivyo masikini.
Ofisi yangu ya Tokyo inapokea CV za Wamarekani 80-230 kila mwezi. Ofisi yetu ya China zilipokea 420 mwaka Jana. Haya ni maombi ya kazi kwenye kampuni moja tu!!!
Kama maisha ni mazuri wananchi wao wasingetaka kufanya kazi nje . Wangebakia na kula bata kwao. Lakini wajanja wanajua, pesa ipo Asia siku hizi.
Uchumi wa China utaipita Marekani muda sio mrefu. Umeshaipita Japan.
Uchumi wa dunia ukitikisika, investors wananunua Yuan na Yen sio Dola na Euro. Kuna sababu wanafanya hivyo.