MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Ninaandika nikiwa na hasira mno kama zile za Mdude kwa CCM ya Magu. Kwa muda mrefu sana nimeshindwa kuelewa ni kwanini wauza vyakula huwa wanatuuzia ugali mlaini karibia kuwa sawa na uji? Yaani unakula ugali tasteless kabisa na unakera zaidi unapoutia mkononi. Kero tupu. Je, ugali mlaini ndo wenye afya? Kwa upande wangu nikila ugali mlaini ni kama sijala kwasababu ndani ya dakika chache nitaanza kusikia njaa.
Tayari nimeshaacha kununua ugali popote na kuelekeza nguvu kwenye vyakula jamii ya ngano na wali. Nikiwa na hamu najipikia mwenyewe mgumu.
Tayari nimeshaacha kununua ugali popote na kuelekeza nguvu kwenye vyakula jamii ya ngano na wali. Nikiwa na hamu najipikia mwenyewe mgumu.