Tafadhali migahawa/hoteli/mama ntilie tupikieni UGALI MGUMU na sio Ugali kama uji

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Ninaandika nikiwa na hasira mno kama zile za Mdude kwa CCM ya Magu. Kwa muda mrefu sana nimeshindwa kuelewa ni kwanini wauza vyakula huwa wanatuuzia ugali mlaini karibia kuwa sawa na uji? Yaani unakula ugali tasteless kabisa na unakera zaidi unapoutia mkononi. Kero tupu. Je, ugali mlaini ndo wenye afya? Kwa upande wangu nikila ugali mlaini ni kama sijala kwasababu ndani ya dakika chache nitaanza kusikia njaa.

Tayari nimeshaacha kununua ugali popote na kuelekeza nguvu kwenye vyakula jamii ya ngano na wali. Nikiwa na hamu najipikia mwenyewe mgumu.
 
Pole Sana, naona upost Facebook ndo Kuna Mama ntilie wengi ujumbe wako utawafikia vzr.
 
Duh kudadeki hili nalo wakalitizame na wapitishe Sheria ni nn hii kunyonyana kama enzi za ukoloni Yani Kati ya ugali na mrenda ,mrenda una afadhali ,ugali sio ugali ugali sio uji dadeki
 
Ikiwezekana achana na ugali, wali na vya ngano. Si vizuri kwa afya. Elekea vya mizizi, kama boga, viazi vitamin, maghimbi n.k.
 
Ikiwezekana achana na ugali, wali na vya ngano. Si vizuri kwa afya. Elekea vya mizizi, kama boga, viazi vitamin, maghimbi n.k.
Asante sana ndugu ila NINAKUAHIDI huu ushauri wako kamwe sitaufuata.
 
Reactions: Auz
Wakipika mgumu watalalamikiwa na wateja kwamba heh ugali wenu mgumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…