Tafadhali naomba mwongozo wa namna ya kufuga Kasuku

Msela Ngoto

Member
Joined
Jun 10, 2018
Posts
29
Reaction score
28
Habari za jioni wanajamvi,

Kichwa cha habari chajieleza hapo juu, wadau nataka kufuga Kasuku lakini sijui naanzia wapi.

Tafadhali naomba mwongozo wenu kwa mtu anayejua chochote kuhusu kasuku, kuanzia upatikanaji wake, chakula chake, makuzi yake pamoja na changamoto nyengine.

Natanguliza shukrani za dhati toka kwenye uvungu wa mtima wangu.

Naomba kuwasilisha.
 
Habari za jioni wanajamvi,

Kichwa cha habari chajieleza hapo juu, wadau nataka kufuga kasuku lakini sijui naanzia wapi.
Tafadhali naomba mwongozo wenu kwa mtu anayejua chochote kuhusu kasuku, kuanzia upatikanaji wake, chakula chake, makuzi yake pamoja na changamoto nyengine.
Natanguliza shukrani za dhati toka kwenye uvungu wa mtima wangu.
Naomba kuwasilisha.
Siti ya mbele kusubiri wajuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wasiliana na ofisi ya maliasili ujue kama vibali vinapatikana kwanza halafu ndio uendelee. pia hapo wanaweza kukuelekeza mahali wanapatikana
 
Ahsante sana mdau kwa maoni yako, angalau sasa nimejua pa kuanzia..
 
Ahsante mdau, ngoja nifanye ili nijue tunakwama wapi.?
Nisije nikafeli kabla ya kujaribu.
Mimi nina connection ya kuwapata wale grey parrot wa congo ambao ndo wenye iq kubwa kuliko spicies zingine ,mmoja anapatikana kwa Tsh 300,000-700,000 kulingana na umri tatizo hawana vibali(magendo) .

Navyosikia watu wanazinunua halafu unamtafuta mwenye kibali ambae zilikufa kisha anajifanya ndo hizo na mnauziana kule maliasili wana transfer kwa jina lako maana vibali havijatoa description unique.
 
Kwakweli umekuwa mdau muhimu sana juu ya jambo langu hili.
turudi kwenye point yako sasa, nadhani sio mabaya tukiwa na matokeo mfukoni coz inaonekana kidogo pana "usumbufu" kupata kibali cha ndege hao.
sasa we fanya hizo connections zako kisha unipe mrejesho tafadhali, nipo "serious" na hili jambo.
usinichoke mdau, natanguliza shukrani kwa ushirikiano wako.
 
Samahani viongozi ni sababu zipi zinapelekea kuwa na vibali ilhali Njiwa na Kanga wangu hawana?
 
Kwakweli umekuwa mdau muhimu sana juu ya jambo langu hili.
turudi kwenye point yako sasa, nadhani sio mabaya tukiwa na matokeo mfukoni coz inaonekana kidogo pana "usumbufu" kupata kibali cha ndege hao.
sasa we fanya hizo connections zako kisha unipe mrejesho tafadhali, nipo "serious" na hili jambo.
usinichoke mdau, natanguliza shukrani kwa ushirikiano wako.
Nimewahi kuwa na wawili mkuu !
siku wtu wakawatonya maliasili waje kunidaka ,tatizo wakiwa mlangoni na geti limefungwa rafiki akanitonya ,nikabidi niwaachilie ,niinbox nkupe namba wako kigoma hata ukitaka kumi
 
Yeah kumbe angalau una experience na hawa ndege, binafsi nawahusudu sana.
Naona ndoto yangu inataka kutimia sasa.
Changamoto iko hapa, mambo ya inbox siyajui i mean PM huwa wanatumaje, msaada please kwa anayejua...
 
Mimi nina connection ya kuwapata wale grey parrot wa congo ambao ndo wenye iq kubwa kuliko spicies zingine ,mmoja anapatikana kwa Tsh 300,000-700,000 kulingana na umri tatizo hawana vibali(magendo) .

Navyosikia watu wanazinunua halafu unamtafuta mwenye kibali ambae zilikufa kisha anajifanya ndo hizo na mnauziana kule maliasili wana transfer kwa jina lako maana vibali havijatoa description unique.
Wanazinunua nini nyanya?zilikufa,ndiyo hizo mnauziana.Mkuu we unazungumzia nyundo au bado uko kwenye kasuku?
 
Back
Top Bottom