changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Kwanzia msimu umeanza kuna kosa kubwa la uchaguzi wa wachezaji hasa eneo la kiungo, na beki hivyo kupelekea timu ya Yanga kutokuwa na utulivu pindi wakishambuliwa. Hii Yanga imekuwa tofauti na ya msimu uliopita ambapo walikuwa wanaenda kushambulia lakini inapopokonywa mpira kila mchezaji anspambana kuwin mpira kwa haraka. Kocha tunaomba kwanza kwenye nafasi ya kiungo patendee haki kwa kumsogeza Bangala nafasi hiyo huyu Birigimana ni mzito hawezi hayo majukumu.