Tafadhali Soma mrejesho huu

Tafadhali Soma mrejesho huu

Nasakadoo

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2014
Posts
343
Reaction score
169
Habari Wadau,Members na Non-Members of JF…
Ni juzi kati tu nilitoka kuweka uzi wa kuomba ushauri au msaada wa kile nilichokieleza.

Baadhi walinishauri pale wengine wakaponda ombi langu ila yote heri tu. Tena nilionana na mwana Jf maeneo ya Ubungo anatumia jina la #Mjasiliamali_Elimu humu, alinipa ushauri wa Mawazo mazuri tuu kilichobaki ni utekelezaji.

Sasa Issue ni kwamba (kwa wale ambao labda hawakuona uzi wangu) nimehangaika saana saana kutafuta ajira au kibarua chenye tija,nimeshindwa,nimehangaika pia kujiajiri lakini sikuwa na mtaji wa kutosha kwa hilo. Ndo nikaja humu Jf kuomba msaada wa kimoja wapo au vyote viwili, bado sijafanikiwa labda nimefanikiwa kwa 40%(kwa msaada wa mawazo).

Sasa hivi nilikuwa na Plan hii, na nakuomba msomaji wa Uzi huu ukonsetreiti hapa;
Ukweli kupata ajira ni ngumu saana… na kujiajiri pia ni ngumu kama huna vyanzo vya uhakika vya mtaji.

Mimi nilikuwa naomba kwa yeyote aliye tayari kunifadhili Bajaj (TVS King) au Noah,naomba tuongee…

Unanipa Bajaj halafu mimi nakuwa nakutafutia hesabu…
Kwa hesabu ya haraka haraka Bajaji kwa siku nitakuwa naleta Tsh10,000 hadi Tsh 15,000 kutegemea na Mazingira ya Kazi.
bahati nzuri nimewahi kuwa dreva bajaji so nina experience na hii shughuli.
Tsh10,000×6 (siku)=60,000/-
Hapo Masuala ya Service ni juu yangu.
Au
Tsh15,000×6(siku)=90,000/-
Hapa Service ni juu ya Bosi.
na Service ya Bajaj kama Dreva ni mzuri inaweza kufanyika mara moja kwa Mwezi au kila baada ya miezi miwili
kwa sababu issue kubwa kwenye Bajaj Slider na Hubcup zake ndo mara nyingi husumbua…

Siku ya 7 nimeitoa kwa sababu binafsi ni mkristo so ningeomba niwe nahudhuria Church na kufanya usafi kidogo ndiyo maana nimepiga mahesabu ya Siku sita sita.

Kwa Upande wa Noah huko Pia ni Maelewano tu,maana kuna maeneo yanakuwa na Abiria wengi na hayana lami… so kwangu mimi location nzuri naijua au itategemea na masharti ya mwenye chombo kujua nimletee hesabu sh ngapi baada ya Makato yoote ya siku.

Nadhani mpaka hapo kuhusu vyombo hivyo nimefafanua vizuri kiasi ambacho mwenye chombo anaweza kunitathimini ili tuonane na kupeana majukumu rasmi.
Nina uhitaji kweli,
Leseni ya Udreva ninayo,ina Madaraja A,B,C,D,& E.
Jinsia yangu ni ME umri wangu hauzidi miaka 27.

Lakini pia la Nyongeza sasa labda huko kote nimefeli,
Mimi pia napenda kuuza Dukani,duka lolote lile,liwe la Hardware,Soft Drinks,Casual Wears,Electronics, la Mchanganyiko wa Bidhaa mimi nipo vizuri,ni suala la kuelekezwa siku moja mbili,then We go.
So kama kuna mtu ana una mtu anatafuta mtu wa hivyo naomba tuwasiliane ndugu zangu.
Pia kuna wale Wanaotafuta Madreva wa kuwa wanawapeleka kazini na kwenye Project mbali mbali,mimi nipo Tayari kuwa Dreva wako… tuwasiliane pia.
Kwa kifupi ni hayo tu,naomba mnifikirie kijana wenu,mwanenu,ndugu yenu,n.k.
Unaweza kuni PM au namba yangu ya Simu ni
+255 718 65 11 74.

NITASHUKURU OMBI LANGU LIKIKUBALIWA.
IN GOD/ALLAH WE TRUST.
 
tatizo vijana mnachagua kazi
Hili ndo tatizo la vijana wa kileo!!

Sisi wengine tulipomaliza vyuo serikali haikuwa na ajira ulikuwa unamaliza unaagwa kama ulivyo kuja, labda tofauti inakuwa tu kwa vile unaondoka na cheti! Tuliingia mpaka kwenye ufundi ujenzi, kubeba zega n.k. Kufika hapa tulipo sasa ni juhudi binafsi. Hivyo huyu mdau kama hachagui kazi mbona zipo nyingi tu humo mjini? Eti kuuza kwenye duka la hardware? Ulishauliza ukuli kwenye mabohari ya akina Kamaka? Kwa akina Wahenga? Piga hata ubeba mizigo kwenye hayo makampuni!
 
Hili ndo tatizo la vijana wa kileo!!

Sisi wengine tulipomaliza vyuo serikali haikuwa na ajira ulikuwa unamaliza unaagwa kama ulivyo kuja, labda tofauti inakuwa tu kwa vile unaondoka na cheti! Tuliingia mpaka kwenye ufundi ujenzi, kubeba zega n.k. Kufika hapa tulipo sasa ni juhudi binafsi. Hivyo huyu mdau kama hachagui kazi mbona zipo nyingi tu humo mjini? Eti kuuza kwenye duka la hardware? Ulishauliza ukuli kwenye mabohari ya akina Kamaka? Kwa akina Wahenga? Piga hata ubeba mizigo kwenye hayo makampuni!

It was my suggestion Mkuu, so sio mbaya hata ukiniitia sehemu hiyo ya kubeba Zege. Mimi nafanya. Trust me,
 
mmemuita uko kubeba Zege akakataa? pia kila mtu na professional yake.

Uwezi kwenda kuomba kazi sehemu ukasema kazi yeyote tu.lazima useme ni kazi gani unazoomba na ulizo na ujuzi nazo.

Mtoa mada yuko wazi kabisa na kaeleza kwa ufasaha na namba za simu kaweka.Natumain watakutafuta
 
mmemuita uko kubeba Zege akakataa? pia kila mtu na professional yake.

Uwezi kwenda kuomba kazi sehemu ukasema kazi yeyote tu.lazima useme ni kazi gani unazoomba na ulizo na ujuzi nazo.

Mtoa mada yuko wazi kabisa na kaeleza kwa ufasaha na namba za simu kaweka.Natumain watakutafuta

Hakika…
 
H
Jamani wana jf nimeamua kuwatia moyo wanaume wote wanaojiona kuwa ni dhaifu kwa sababu ya kukosa kipato, mapenzi n.k.

Kuzaliwa mwanaume ni ushindi tosha kwani idadi ya mifuko uliyonayo kwenye mavazi yako iwe suruali au shati inakufanya uwe superior mbele ya jamii, inakuongezea nguvu hata kama huna fedha bado watu watakuwa na uwezo wa kubashiri kwamba kama si mfuko wa mbele basi wa mfuko wa nyuma lazima atakuwa na ela.

Kwa hiyo usijione inferior mbele za wenzako kwani idadi ya mifuko uliyonayo inakupa confidence ya kukabiliana na jambo lolote hiyo ndio tofauti kubwa iliyopo kati yetu na wenzetu. Hivi umeshawahi kuona vazi la kike lina mifuko mingi kuzidi vazi la mwanaume. hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini wanawake wengi simu zao wanashika mkononi.

Jivunie kuzaliwa mwanaume kwani hata vitabu vitakatifu vinatoa sifa za pekee kwa mwanaume, na nachukia sana tabia za baadhi ya wanaume kusema " afadhari ningezaliwa mwanamke ningekuwa nafanya kazi ya kumuoshea Mume wangu nguo" hayo ni mawazo mgando .

Jivunie kuzaliwa mwanaume pamoja na changamoto ulizonazo.

Najivunia kua mwanaume
 
Mkuu hongera kwa jinsi ulivyojieleza, natamani ningekuwa na uwezo wa kukusaidia ila kwa ufupi ni bajaj ila si aina ya tavez ni zile za zamani na niliamua kuipaki kwa kufanyiwa uhuni na vijana unao waamini, waliiba injini wakaleta na longo longo kibao na niliponunua injini mpya nikaifunga nilipata dereva mwaminifu kwa muda sema akaamua kurudi kijijini tokea hapo nikaipaki mpaka leo.,kama unahisi hii yaweza kusaidia ni pm na wala sihitaji makubwa ktk hili ila kama uko specific na hitaji la tavez basi njoja ikae tu hapo.,.nb sina nia nikuajiri bali ujiajiri kupitia iyo bajaj kama itakufaa..samahani kwa maneno mengi
 
Uweke wazi na watu wa kukudhamini,
duniani imani imekwisha.

wewe nawe unaonekana ndo wa kwanza kuishiwa na Imani hapa Duniani maana comment zako nyingi ni umebase hapa ''Imani imekwisha'',....
 
Back
Top Bottom