Tafadhali wadau naomba mnisaidie 5m Tshs nikakomboe hazina

Status
Not open for further replies.

CORAL

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2011
Posts
2,813
Reaction score
1,827
Wana JF nina jukumu moja kubwa la kuhamisha hela kutoka benki moja kule Scotland UK ili nizihamishie benki ya hapa Tz tawi moja la NBC. Ni zoezi ambalo limepitia mchakato mrefu kiasi na sasa niko katika hatua ya mwisho ili hela zitumwe. Kinachonikwamisha kufikia sasa ni kwamba natakiwa kumtuma mwanaseria wangu ambaye ameshughulikia hilo suala toka mwanzo ili akasaini documents fulani zinazohusiana na uhamshaji wa hizo hela. Yaani hayo ni masharti ya benki husika kwa mujibu wa sheria za Uingereza. Kiasi cha hela ninachohitaji kwa sasa ni sh. 5m (zingine zipo).
Naomba ieleweke kwamba hiki ni kitu halisi sio utani na documents zote ninazo nasubiri tu kukamilisha kazi iliyobaki hela zituwe. Nilikuwa ninasita kuja hapa maana watu kuamini vitu kama hivi ni ngumu sana unless mnaongea ana kwa ana. Nimejaribu kitafuta hela huku Mbeya nilipo tangu novemba 2013 lakini sijafanikiwa kukamilisha na muda unaenda tu. Kifupi mimi ni mtumishi wa serikali na sina fursa yoyote ya kuomba mkopo maana nimeishatumia kiasi cha pesa kuprocess documents za kuniwezesha kumiliki hiyo hazina.
Naomba wakuu zingatia kwamba nikipata hiyo hela ni zoezi la ndani ya wiki 2 tu ili hela zitumwe. Atakayenisaidia atalipwa hela yake 5m na ziada.ya 5m jumla milioni 10. Zaidi ya hapo tutawasiliana nijue shughuli anazofanya kuna upungufu gani ili nimpe support. Kimsingi nitamfanya awe mdau wangu na kupeana ushauri wa mambo ya kibiashara.
Najua kuwa maelezo yangu yanaacha maswali fulani ya msingi sana lakini nitafafanua kwa yeyote ambaye yuko interested kunisaidia. Kinachotakiwa ni kuni PM ili tuongee biashara au nitafute kwa namba hii 0755144512. Details nitazitoa in private tafadhali. Nawasilisha
 

Pole sana kwa matatizo yaliyokupata ndg yangu pesa ni kitu kingine kabisa watu sasa hivi wameshapoteza iman watu wanataka uweke kitu rehan akupe hela hapo utapata ila useme mtu akupe tu bila dhamana hapo utachemka
 
Huna collateral yeyote? Au ndugu akuthamini ungepewa mikopo binafsi ya dharura watu kukuamini ngumu
 
weka dhamana + kuandikishiana police hela bana ni kitu ingine kabisa katika maisha
 
kuna maelezo yako yameweka maswali ungeweka na majibu yake ingekuwa rahisi somehow!
 
Naomba nikupe angalizo ndugu yangu. Kama hao watu walikuja na gia ya kukuambia mwenye akaunti alikufa ila taratibu zote zimefanyika ili pesa ziingie kwako na baadae mgawane, jua ya kwamba umeingia kwenye mikono ya matapeli. Ukituma tu hizo hela umekwisha, utajuta kuwafahamu.
 
By CORAL:

Atakayenisaidia atalipwa hela yake
5m na ziada.ya 5m jumla milioni
10. Zaidi ya hapo tutawasiliana
nijue shughuli anazofanya kuna
upungufu gani ili nimpe support.


Hapa ndipo watakapo umia wengi...
 

Wizi wa ki-nigeria, moderator Ondoa hii kitu na piga burn aliyeleta topic
 
CORAL umepigwa au ndo unajifunza kupiga hapa jf...
 
Last edited by a moderator:
By CORAL:

Atakayenisaidia atalipwa hela yake
5m na ziada.ya 5m jumla milioni
10. Zaidi ya hapo tutawasiliana
nijue shughuli anazofanya kuna
upungufu gani ili nimpe support.


Hapa ndipo watakapo umia wengi...

Huyo jamaa ni tapeli tu. Umkopeshe akulipe mara2 ya pesa ko dunia ya wapi hiyo
 
Kumbe ww ni mtumishi wa serikari, mbona mambo kwako mepesi tu, nenda haraka Baypot with your recent salary slip within 24 hrs you will have cash in hand.
 
Duh!!! Wizi Wa Kizamani, Kuweni Makini Jamani Msije Mkajuta Kuzaliwa
 
Huyu mnamuonea bure jamani, yeye si tapeli ila ameingia mikononi mwa 'wapopo'. Atakuwa ameshaliwa kidogo kidogo sasa wazee wa kazi wanataka kumpiga ya ukweli, Bro achana na hiyo mambo, maisha sio mepesi hivyo, fanya kazi kwa bidii achana na hayo mambo sijui mtu alikufa ana hela nyingi bank wanatafuta mrithi, shtuka na uachane nayo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…