Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tiba yake ni kufanyiwa upasuaji mdogo ikaondolewa. niliisha wahi kuwa mhanga. maumivu makali ya tumbo hayaelezeki mpaka unaona vimulimuli:bowl::bowl::bowl:
Dalili zake zaweza kuwa nyingi ngoja waje.
du basi ya kwangu naona ilizidi hapo kabla haijagundulika nilishaumwa tumbo kama mara mbili na kulazwa na sio siri na nilikuwa na maumivu makali balaa kiasi cha kuona hivyo vimulimuli na kutapika balaa. cha ajabu mwanzo mara wanitibu typhodi mara marelia kumbe hivyo vyote sina at last mara ya tatu maumivu yaligoma kupoa si kwa drip, oksjeni, dawa za usingizi sijui za kutuliza maumivu vyote vilishindikana kwa kweli nilikuwa na maumivu makali sana mpaka mwisho kugundua ni apendix. So uzoefu wangu mimi ni maumivu makali niliyoyapata.kuna wakati maumivu yanakua sio makali kihivyo.kuna na maumivu kwenye tumbo upande wa chini kulia.yanaweza kuwa yanakuja na kwenda ,yakawa makali au kwa mbali,ila ujue kuna Acute appendex na chronic appendex. Ikiwa bado acute itakua inakusumbua na kupoa na wakati mwingine haiumi sana lakini unajua tu something is wrong there. Then kuna siku itakukamata kiasi utashindwa hata kutembea wima,hata kukohoa au ukipiga hatua hiyo sehemu inauma hiyo stage ndo chronic appendex inabidi uitoe kwani inakua imeshavimba na iko na infection na inaweza kupasuka na ikipasuka itakuchukua muda mrefu sana kupona au hata usipone ukafa. Haya ni maelezo kufuatana na uzoefu wangu kwani nilifanyia operation ya appendex wiki tatu zilizopita na naendelea kurecover.