Tafadhalini viongozi wa Simba Kibu Dennis arudi haraka sana kuokoa jahazi, Singida anatengenezewa mazingira ya kushika nafasi ya pili juu ya Yanga

Unaongea utadhani Simba ana haki ya kutawala wapinzani nyakati zote, pia unawadharau JKT ambao kabla ya Simba haikufungwa mechi tano zilizopita,Simba unayoona inacheza vibaya ndio timu inayoongoza kufunga magoli mengi, imefungwa machache kuliko timu yoyote, inaongoza ligi na imepiga pasi nyingi kuliko timu yoyote. Umeangalia udhaifu wa Mutale tu na kusahau kuwa hata Yanga kuna wachezaji wengi viwango vimeshuka wakiwemo Aucho,Aziz na Baca ambaye rate ya kucheza faulo za kadi nyekundu ni nyingi tu, mechi iliyopita ni huruma ya refa tu hakupewa kadi ya pili ya njano pale alipofunga goli la mkono wakati anayo tayari kadi ya njano.
 
Mwaka unaenda mbio Sana. Simba Leo wanamtegemea Kibu Denis!?
Kwani huyu aliendika ni nani kwenye timu ya Simba hadi uchukue malalamiko yake kama ni ya Simba?
 
🤣Yanga Yes ni imeshuka kiwango kutokana na kuwa peak sana ....Kuwa na goli nyiingi au kufungwa chachee si kigezo Mfano Natumia mfano wa Nje Bayern Munich ni tishio Ujerumani ila ukikutana nayo Uefa inakuwa unga......Narudi Bongo Simba yes ana perform ila Kuna namna timu hata ikifungwa unaona hii timu inakitu ....Nakupa mfano mwingine Derby ya kwanza Simba alifungwa na Yanga ila alikuwa na uhai tofauti na ya ligi kuu...

Kuhusu mchezaji kama Baka timu yake imefungwa game 1 TU akiwemo NBC ila nyingine zote anaperform..Namlinganisha na Chemalone ni mzuri ✅✅ ila anacheza sana lawama zinaanza hana kiwango,mara ameshuka ila tunaoangalia tunajua huyu ni balaa rekebisha mtazamo hapa..

Jkt ni wakawaida wewe kwa timu kama Simba ,Game 5 ana goli 2 ,mech nzima mmetawala ila Rudia maelezo yangu ya pale juu na nakuongezea hii kuna namna hata kocha akifanya sub hazilete madhara ya Moja kwa moja
 
Labda kama humwangalii Baca kwa makini, siku hizi anaruhusu sana kupitwa, halafu akipitwa anavuta na kukumbatia sana wachezaji, hata mechi ya juzi alivuta mara mbili, katazame mechi vs Al Hilal goli la kwanza, yeye huwa mzuri kwenye sliding takles, siku hizi ni kama wamemjulia. Mchezaji anayemfutia makosa ni Job ambaye kwangu ndiye beki bora wa kati kwa sasa NBC.Unalaumu sub za Simba lakini umeshindwa kuona kuwa baada ya kuingia Ahoua na Zimbwe mpira ulibadilika na Simba kuzidisha mashambulizi hadi kupelekea JKT kufanya makosa kwa sababu pressure ya mpira ilikuwa juu,kwa sababu humpendi Mutale na uliangalia mpira kwa jicho la ukosoaji hivyo ulikuwa unatafuta makosa ya Mutale badala ya kuangalia subs wengine wanafanya nini.Umeshindwa pia kuiona fact ya kucheza mechi kila baada ya siku mbili inayochochea fatique kwa wachezaji wa Simba, yaani ni kama umeipa Simba hatimiliki ya kushinda na kucheza vizuri dhidi ya timu zote 15 na umesahau kuwa hii ni ligi na timu zote zimejiandaa kushindana
 
Naanza na Baka....Umesema kabisa Aucho kashuka kiwango alafu baka anapitwa unaona hoja Yako ya fatique inapoingia ...Ngoja Nije kwenye takwimu kabisa tumalize hili
•NBC Simba kafungwa goli 5,Yanga kafungwa 6(3 vs Tabora,2 vs Mashujaa na 1 vs Azam....Bacca unaemlalamikia Kawepo kwenye game Moja TU ya mashujaa(Ya juzi waliofungwa 2 ile michomo)....Kupitwa kupo tu sikatai ndio mana lazima Namba 6 afanye back up, Baka kama takwimu zilivyo hapo karuhusu goli 2 na 1(ntasema Ile ya Azam) ila akikosekana acheze mamnyeto ndo utaona utofauti mamnyeto anashika,anakukwatua ...Pia labdah tu goli la juzi likikukera ila kwa Yanga mchezaji anayeongoza kwa hayo uliyoyasema hapo juu ni Aucho(Anashika,faulo za kijinga n.k)To you Job ni Bora ila to us Baca ni next level asee hana makosa mengi kama unavomshuku.....Kimataifa Chemalone Juzi kazinguwa zaidi ya mara tatu ila waarabu hawakuwa smart ila walipata dodo chini ya mnazi so Game na al hilal kosa la bacca ni la kawaida tu upande wangu

--Sub za Jana usiongee lolote maana nimeshasema timu yenu ilitawala mchezo mfano upande wa zimbwe, Nouma alikuwa powa sana mda wote ila alipoumia zimbwe aliingia kuendeleza tu,Ahoua ngoja nikae kimyah ila mm nahitaji mda maana kiuchezaji namfananisha na Aziz ki ni mchezaji wa kipindi maalumu hakuwa na impact hiyo maana penalty ww ni shahidi uzembe wa beki umeicost timu...
 
Nimezungumzia pressure ya mchezo iliongezeka baada ya Ahoua kuingia, kaangalie vizuri hata ile pasi iliyosababisha beki akamvuta Kapombe, beki mwingine aliunawa mpira uliotoka kwa Ahoua hivyo penati ililuwa haiepikiki, hii yote ni sababu ya Ahoua, kufanya makosa kwa Che Malone hakufuti makosa ya Baca, sema una mapenzi makubwa na Baca kiasi huoni makosa yake, siku hizi ni mdhaifu hata kwenye set piece,anaruka kwa macho, pia anajichanganya sana, ile mechi dhidi ya MC Alger goli la pili ni uzembe wake, makosa haya hatujayazoea kwa Baca.Jiulize mwaka jana wakati kama huu Yanga ilikuwa imefungwa magoli mangapi na sasa mangapi, Baca alikuwa na blanders za namna hii?
 
Huyu Baca unayemsifia kama si udhaifu wa washambuliaji wa timu pinzani Yanga wangekuwa wanafungwa magoli mengi tu,goli la pili dhidi ya MC Algers na hii situation inadhihirisha hili
 

Attachments

  • KIDOGO WAUWANE __😜(MP4).mp4
    930.3 KB
Huyu Baca unayemsifia kama si udhaifu wa washambuliaji wa timu pinzani Yanga wangekuwa wanafungwa magoli mengi tu,goli la pili dhidi ya MC Algers na hii situation inadhihirisha hil
😀Sawa ila uzembe umeanzia upande ganii mkuu....Kosa la bacca hapa likwapi
 
Sawa ngoja nikubali ana makosa ila makosa katika game yapo Tu ...sababu b4 game ya MC Alger na al hill kumbuka Yanga hakufungwa ata goli la mkono
 
Kibu ana magoli mengi ya CAF msimu huu kuzidi kikosi kizima cha Uto
Uko shirikisho ata ufunge Goli 100 hazina thamani ilo ni kombe la kina mama.
Kama kweli Kibu ni mkali wa nyavu, NBC premier league ana Goli ngapi?
 
Sawa ngoja nikubali ana makosa ila makosa katika game yapo Tu ...sababu b4 game ya MC Alger na al hill kumbuka Yanga hakufungwa ata goli la mkono
Kwani mechi na Azam na Tabora zilichezwa after MC Algers na Al Hilal?
 
Kwani mechi na Azam na Tabora zilichezwa after MC Algers na Al Hilal?
Gusa achia twende kwao 4G bado goli 4 😄😄timu yenye goli nyiingi ifikiwe ,taratibu taratibu

..Sikumbuki ila nakumbuka Job na Bacca hawakuwemo game ya Tabora
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…