Tafadhari Endesha Kwa kujihami

Tafadhari Endesha Kwa kujihami

CHIBA One

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2018
Posts
558
Reaction score
2,093
Wamiliki wa magari wameongezeka, siku hizi kila Mtu ndoto Yake ni kumiliki gari, Miongoni Mwao kuna madereva wabaya, kuna waliojifunzia uchochoroni baada ya Wiki anaingia barabarani...

Nje Ya hapo kuna Bodaboda, kuna watu wanaotembea na stress/ depression, kuna waendesha baiskeli, kuna malori n.k

Juzi Mida ya jioni Natoka zangu sehem nawahi Nyumbani nikiwa town bado, Maza Mmoja alikatisha barabara ghafla sana akiwa wala haangalii hatari kushoto wala kulia kwake, na mimi nilikuwa nimeiva sana japo haikuwa above 70 kph.aisee mita 3 mbele ghafla kaingia Road, namna nilivyomkwepa nahisi ni kwa Uwezo wa Mungu tu...lakini nilikuja kugundua alikuwa na mawazo sana..

Funzo la kuendesha kwa kujihami niliona lina umhimu sana...Bado kuna bodaboda ambao muda wote anaweza kukusababishia chochote. vijana wetu hawa wakishalewa nao na yuko Ndani ya chuma na demu wake basi haelewi lolote ni speed na mziki mkubwa ulevi na kuendesha umekatisha maisha ya jamaa zetu wengi. Tuwe makini.
 
Kwa kweli… mzidishe umakini

Hata sisi watembea kwa miguu tuwe makini sana, haswa ndugu zangu waarusha, nyie watu hamuogopi magari na uwa mnangoja gari ikupishe wewe . Mbadilike
Wanasubiri tuwagonge ili wadai fidia. Nikigonga naua tu.
 
Mimi baada ya kupata mtoto mwanzoni mwa mwaka huu nathamini sana maisha. Naendesha kwa umakini sana labda itokee tu dharula.

Kuendesha gari Dar es Salaam ni changamoto kubwa sana, kushito kuna bodaboda, kulia kuna bodaboda, bajaji, daladala, watembea kwa miguu, mbaya zaidi kwenye barabara hizi za one way. Angalau barabara mbili wote mnarlekea upande mmoja kuna unafuu.

Barabara za Dar, ukisema ukwepe shimo uingie kushoto kidogo, kuna boda oda utamsukuma mtatoni, kulia kuna guta ni shida tupu.

Usiku sasa ndio changamoto kubwa, full lights kila kona. Ni changamoto sana.

Tuongeze umakini tulinde maisha barabarani.
 
Wamiliki wa magari wameongezeka, siku hizi kila Mtu ndoto Yake ni kumiliki gari, Miongoni Mwao kuna madereva wabaya, kuna waliojifunzia uchochoroni baada ya Wiki anaingia barabarani...

Nje Ya hapo kuna Bodaboda, kuna watu wanaotembea na stress/ depression, kuna waendesha baiskeli, kuna malori n.k

Juzi Mida ya jioni Natoka zangu sehem nawahi Nyumbani nikiwa town bado, Maza Mmoja alikatisha barabara ghafla sana akiwa wala haangalii hatari kushoto wala kulia kwake, na mimi nilikuwa nimeiva sana japo haikuwa above 70 kph.aisee mita 3 mbele ghafla kaingia Road, namna nilivyomkwepa nahisi ni kwa Uwezo wa Mungu tu...lakini nilikuja kugundua alikuwa na mawazo sana..

Funzo la kuendesha kwa kujihami niliona lina umhimu sana...Bado kuna bodaboda ambao muda wote anaweza kukusababishia chochote. vijana wetu hawa wakishalewa nao na yuko Ndani ya chuma na demu wake basi haelewi lolote ni speed na mziki mkubwa ulevi na kuendesha umekatisha maisha ya jamaa zetu wengi. Tuwe makini.
"Umeiva sana" chini ya 70kph?

Bro, walioiva sana wanaanzia 130kph kuendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kweli… mzidishe umakini

Hata sisi watembea kwa miguu tuwe makini sana, haswa ndugu zangu waarusha, nyie watu hamuogopi magari na uwa mnangoja gari ikupishe wewe . Mbadilike
Aisee ila watembea kwa miguu wa Arusha 🙌🙌
 
Kwa hapa DAR speed 70 ni kubwa Sana kwenye maeneo mengi ebu fikiria upo mitaa ya kariakoo barabara ya msimbazi alafu uko hiyo speed au upo mitaa ya buguruni mnyamani...
Barabara za DAR ni hatari Sana hasa kama upo speed 50 nakuendelea
"Umeiva sana" chini ya 70kph?

Bro, walioiva sana wanaanzia 130kph kuendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hapa DAR speed 70 ni kubwa Sana kwenye maeneo mengi ebu fikiria upo mitaa ya kariakoo barabara ya msimbazi alafu uko hiyo speed au upo mitaa ya buguruni mnyamani...
Barabara za DAR ni hatari Sana hasa kama upo speed 50 nakuendelea
1. Sijaona sehemu alisema alikuwa dar.

2. Huwezi enda 70kph kkoo kwasababu hutapata hiyo nafasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom