TheRealOdyssey
New Member
- Jul 22, 2026
- 1
- 0
TheRealOdyssey!
Ninaandika kwa heshima kubwa na kwa nia njema ya kuona elimu katika halmashauri ya Musoma ikipiga hatua na kuwa mfano wa mafanikio katika Mkoa wa Mara na Tanzania kwa ujumla.
Kwa muda mrefu kumekuwa na hali ya kutoridhisha katika matokeo ya mitihani ya kitaifa na hata ya kikanda kidato cha Pili na Nne katika shule zetu zinazohudumiwa na halmashauri ya Musoma. Kinachotia hofu zaidi ni kwamba hali hii imekuwa ikijirudia mwaka hadi mwaka, bila kuonekana kwa mabadiliko makubwa yanayolingana na juhudi zinazofanyika katika sekta ya elimu.
Jambo la msingi ambalo tunapaswa kujiuliza; Ni kwa nini hali hii imeendelea kujirudia? Chanzo cha tatizo ni nini, na kwa nini hatua madhubuti hazijachukuliwa ili kulitatua?
Ni muhimu viongozi wa elimu katika halmashauri ya Musoma kufanya tathmini ya kina na ya dhati kuhusu sababu zinazo sababisha shule zetu kufanya vibaya katika mitihani ya kitaifa na kikanda. Hatupaswi kusubiri matokeo yatoke ndipo tuanze kulaumiana. Tunahitaji mfumo wa kutambua mapema changamoto, kuzifanyia uchambuzi na kuchukua hatua kabla ya matokeo ya mitihani.
TheRealOdyssey, anakiri kuna baadhi ya wakuu wa shule ambao, kwa kutambua changamoto zao wenyewe katika uongozi, wamewahi kueleza wazi kuwa hawajisikii kuwa na uwezo wa kutosha wa kuongoza shule wanazozisimamia na wameomba kupisha nafasi hizo ili wapewe viongozi wengine wenye uwezo, nguvu mpya na mbinu tofauti za kuendesha shule. Hili linapaswa kuangaliwa kwa jicho la hekima na kwa maslahi mapana ya elimu.
Kumlazimisha kiongozi kuendelea kushikilia nafasi ambayo yeye mwenyewe anaona hana uwezo wa kuimudu ipasavyo siyo suluhisho la tatizo. Ikiwa kiongozi ameomba kuondolewa kwa sababu anaona hawezi kutoa mchango unaotarajiwa, ni muhimu ombi lake lisikilizwe na kutathminiwa kwa uadilifu. Uongozi siyo nafasi ya kushikiliwa kwa lazima, uongozi ni dhamana inayopaswa kutolewa kwa mtu mwenye uwezo, utayari, maono na mbinu za kuleta matokeo.
TheRealOdyssey; anaona ni muhimu kutambua kwamba kuinua taaluma kunahitaji uongozi imara, umoja, ushirikiano, mawsiliano mazuri na nidhamu ya kazi.
Katika baadhi ya shule, changamoto za kitaaluma zinaweza kuwa zinachangiwa pia na udhaifu katika uongozi na usimamizi wa rasilimali watu. Kiongozi mzuri wa shule hapaswi kutafuta kuogopwa na walio chini yake, bali anapaswa kujenga heshima kupitia haki, hekima, ushirikiano na mfano bora wa utendaji. Uongozi wa kuwatisha watu unaweza kuzalisha ukimya, lakini hauwezi kujenga moyo wa pamoja wa kufanya kazi kwa bidii.
Kiongozi anapaswa kuwaunganisha walimu wake, kuwahamasisha, kuwasikiliza na kuwafanya wajione kuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya shule. Walimu wakiaminiwa, wakiheshimiwa na kuunganishwa katika lengo moja, uwezekano wa kufikia matokeo mazuri huongezeka.
Ni jambo la kusikitisha kuona wakati mwingine viongozi wanatumia muda mwingi kujenga makundi na kuwasemea baadhi ya watumishi kwa viongozi wa juu, badala ya kutumia muda huo kutafuta suluhisho la changamoto za kitaaluma. Tabia ya kumchafua au kumsemea vibaya mtumishi mbele ya viongozi kwa sababu tu ya kutokubaliana naye haiwezi kujenga taaluma. Badala yake, huongeza migogoro, hujenga chuki na kuharibu umoja wa watumishi.
Taaluma haiwezi kujengwa kwa misingi ya visasi, makundi, upendeleo au hofu. Taaluma hujengwa kwa haki, uwajibikaji, ushirikiano, upendo wa kazi na uongozi wenye maono.
Kwahiyo, TheRealOdyssey; anaomba viongozi wa elimu wa halmashauri ya Musoma wafanye tathmini ya kina kuhusu hali ya elimu katika shule zetu. Tathmini hiyo isiishie kwenye kuangalia alama za mitihani pekee, bali iangalie pia;
1. Uwezo wa utendaji wa viongozi wa shule.
2. Mazingira ya kazi na mahusiano kati ya walimu na viongozi wao.
3. Uwezo wa shule kupanga na kutekeleza mikakati ya kuinua ufaulu.
4. Matumizi sahihi ya takwimu za mitihani katika kubaini maeneo yenye udhaifu.
5. Ushirikiano kati ya walimu, wazazi, wanafunzi na viongozi wa elimu.
6. Sababu zinazo sababisha shule zetu kufanya vibaya kwa muda mrefu bila mabadiliko makubwa.
7. Uwezo wa kila kiongozi katika nafasi aliyokabidhiwa na kama ana mbinu na utayari wa kuleta mabadiliko.
TheRealOdyssey; anakumbusha tusiridhike na hali ya sasa. Matokeo mabaya yanayojirudia mwaka hadi mwaka, ni ishara kwamba kuna tatizo linalohitaji uchunguzi na hatua za kimkakati kuchukuliwa. Hatupaswi kuzoea kushika nafasi za mwisho kana kwamba ni jambo la kawaida. Kila matokeo mabaya yanapaswa kuwa sababu ya kujiuliza tulikosea wapi, nini hakikufanyika vizuri na tufanye nini tofauti katika mwaka unaofuata.
Ni wakati sasa wa kusikiliza walimu na wakuu wa shule wenye malalamiko ya msingi kuhusu changamoto za uongozi. Wale wanaoona kuwa hawana uwezo wa kuendelea na nafasi zao wanapaswa kusikilizwa. Vilevile, wale wenye uwezo, maono, utayari na mbinu mpya za kuinua taaluma wapewe nafasi ya kuonyesha uwezo wao.
Mwisho, huu siyo ujumbe wa kumshambulia mtu binafsi, bali ni wito wa kutafuta suluhisho la changamoto inayotugusa sote. Elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii. Watoto wanaosoma katika shule zetu leo ndiyo viongozi wa kesho. Kwahiyo, hatupaswi kuacha changamoto za uongozi, migogoro ya ndani au udhaifu wa usimamizi kuendelea kuathiri mustakabali wa wanafunzi wetu.
TheRealOdyssey; anahimiza viongozi wa juu waangalie kwa jicho la huruma, hekima na uwajibikaji hali ya elimu katika halmashauri ya Musoma. Tuwasikilize walimu. Tuwasikilize wakuu wa shule. Tuwape nafasi viongozi wenye uwezo na utayari wa kuleta mabadiliko. Na zaidi ya yote tujenge utamaduni wa kufanya kazi kwa umoja, heshima na ushirikiano.
Musoma inaweza kufanya vizuri. Shule zetu zinaweza kufanya vizuri, walimu wetu wanauwezo wa kufanya vizuri. Kinachohutajika ni uongozi wenye maono, mikakati sahihi, uwajibikaji na utayari wa kufanya mabadiliko.
TheRealOdyssey!*