Mgeni wa Jiji
JF-Expert Member
- Jul 27, 2017
- 9,758
- 18,431
Wasalaam JF
Nimejaribu kufuatilia vituo vingi vya habari na hata mazungumzo ya baadhi ya maeneo niliyopo na kushtushwa na kupotea kwa umaarufu ya sikukuu ya wakulima 8/8.
Katika fuatiloa yangu nimegundua kuwa mechi ya juzi ya watani wa jadi ni kama nayo imepigilia msumari wamoto kwenye kufichwa kwa sikukuu hii ya wakulima.
Vituo vingi hadi leo bado vinachambua na kuzungumzia mechi ya watani Simba na Yanga. Nimebahatika kusikia jambo moja tu likiongelewa tena ni kauli ya Mheshimjwa raisi wa JMT juu ya gharama za magari ya serikali.
Sijasikia jambo lolote juu ya mbolea za ruzuku, vijana wasomi kutoka vyuo vya kilimo na ufugaji, mipango ya wizara na serikali kwa ujumla wake juu ya miradi ya kilimo au hata mijadala ya kilimo tulipotoka, tulipo na tuendapo.
Mbaya zaidi ukiongelea kilimo na maswala yake unaonekana mtu mshamba usiojua lolote la maana.
Ipo midahalo ya michezo kibiashara mingi sana kwa sasa lakini hata hii wiki ya wakulima imeshindikana wizara kufanya mijadala na kuipa promo kweli?
Nadhani huu ulikuwa muda wa kuona yatokanayo na ule mradi wa wizara kwa vijana lakini nao wapi, umefichwa mbali kabisa na jamii yetu.
Natafakari, hivi kweli kilimo kimetushinda au tumeamua kuachana nacho na kufanya mambo mengine.
Ikizingatiwa karibu 70% ya watanzania wanajishughulisha na shughuli za kilimo.
Nadhani ni muda tuwaze upya tunapoelekea kama taifa, hatari ipo ya Tanzania kuwa taifa lenye watu wa hovyo.Afrika mashariki miaka 20 ijayo, pengine hata tukatawaliwa na wenzetu hawa wa hii jumuiya.