KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 3,250
- 5,509
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kulilinda taifa letu dhidi ya maadui wa ndani na nje ambao mara zote wamekuwa mstari wa mbele kuhahakikisha taifa hili halipo salama. Nampongeza Rais wetu na serikali anayoiongoza kuhahakikisha maendeleo yanapatikana na tunasonga mbele kama taifa. Pia, napenda kuwapongeza watanzania wenzangu kwa kudumisha amani, umoja na mshikamamo kulinda maslahi ya nchi yetu.
Moja kwa moja niende kwenye mada, lakini kabla ya kusema chochote ningependa kuuliza swali: Kama mbowe na CHADEMA hawajawahi kumkubali Rais Magufuli, iweje watake maridhiano? Kuna umuhimu wa hayo maridhiano kweli? Naomba tujiulize maswali haya huku tukiendelea kujadili kwa marefu na mapana kuwa maridhiano aliyosema mbowe ni janja ya Mbowe na ni mtego ulioshindwa kumnasa JPM.
Maridhiano ni nini? Maridhiano au upatanisho ni kurejeshwa kwa urafiki , maelewano na uhusiano baada ya kutokea utengano. Je, ni kweli kuna uadui, kukosa maelewano na kufifia kwa mahusiano baina ya CCM na upinzani au Rais Magufuli na Mhe.Mbowe kunakohitaji maridhiano? Huu ni ujanja wa kwanza wa Mbowe kuomba yafanyike maridhiano huku akijua hakuna uadui, kukosa maelewano na badala yake ametengeneza mazingira ya kuonesha hivyo vitu vipo ili kama Rais wetu akikubaliana naye ionekane ni kweli upinzani unaonewa. Huu ni mtego ila umeshindwa kumnasa JPM.
Maneno yanayotolewa mara kwa mara na Rais wetu kuwa maendeleo hayana chama ni ushahidi tosha kuwa kwa kipindi kirefu Rais alikuwa na nia ya kuwashirikisha wapinzani katika maendeleo ila walionekana kupinga na kubeza . Leo kwa nini watake maridhiano huku walionesha kutotaka kushirikiana naye? Binafsi bado sijafikiria kuwa alichokuwa anakiongea Mbowe kakimaanisha ila kakusudia jambo lake mwenyewe.
Kama mlikuwa na nia na kusudi la dhati la kufanya maridhiano mngeanzia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa baada ya wagombea wenu kukosea kujaza fomu kwa makosa mbalimbali. Je, maridhiano ni kukiri mmetambua kosa hili? kama mmekiri mkiri mbele ya dunia kwamba ule uchaguzi ulikuwa ni wa huru na haki na ninyi wapinzani(CHADEMA) tulikosea kuubeza uchaguzi ule, kama mtashindwa kukiri hivi mnataka maridhiano ya nini?
Tanzania ni nchi yenye amani, umoja na mshikamamo na zaidi ya yote imetoa uhuru mkubwa wa vyama vyote kushiriki uchaguzi wa kidemokrasia bila kujali ukubwa au udogo wake, wingi au uchache wa wanachama wake. Mlipoanza kushiriki siasa za kubeza huku msingi ukiwa migomo na maandamano tuliwaambia juu ya hatima ya siasa zenu, mkaweka pamba sikioni hamkutaka kusikia, leo mmesambaritika na kufutika na watu kuchoka siasa zenu mnataka maridhiano. Mnataka maridhiano ya nini sasa? Kwamba mpewe vyeo? Maana jukwaani hamuwezi kusimama mkashinda.
Mapendekezo kwa maridhiano:

- Maridhiano na upinzani yajikite kwa upinzani kufuta kauli zao mbaya zote dhidi ya Rais wetu na wakiri hilo waziwazi bila kificho
- Maridhiano na upinzani yajikite katika kukubaliana na matokeo ya uchaguzi wowote na kukubaliana kushirikiana na chama kinachoshinda.
- Maridhiano na upinzani yatoe mwongozo wa aina za siasa wapinzani wanazotakiwa kuzifanya.
- Maridhiano na upinzani wakiri waziwazi kuwa wamefanikisha kuhujumu jitihada nzuri za Rais za ujenzi wa taifa letu.