Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kwanini Kongo- Kinshasa Kunafukuta?
- Ubia wa Kabila na Tchisekedi u-mashakani
- Kuilewa Kongo- Kinshasa Lazima Uumize Kichwa
- Kabila ( Baba) alimwandaa Mwanawe Joseph tangu Kunduchi Mtongani, Tanzania.
Ndugu zangu,
Mwezi Januari mwaka jana niliandaa mfululizo wa makala kuhusu Kongo- Kinshasa, huitwa pia DR-Congo.
Ilivyo Afrika moto unaowaka nyumba ya jirani yako ni wako, ukishindwa kushiriki kuuzima unaweza kuhamia kwako.
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu yanayotokea Kongo- Kinshasa. Kumekuwa na machafuko kule Beni, Ituri na kwengineko Kaskazini Mashariki ya Kongo - Kinshasa.
Waasi w ADF ( Alliance for Democratic Force) wamekuwa wakifanya mauaji ya kikatili dhidi ya raia. Raia nao wameligeukia jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa ( Monusco)
Monusco kama jeshi lina miaka 21 ndani ya Kongo- Kinshasa. Kuna hoja, kwamba lifungashe na kuondoka.
Swali, kama jeshi hilo linaondoka, ni nini kitatokea Congo bila MONUSCO?
Ni Kongo- Kinshasa yenye majanga ya ebola, surua na waasi wapiganaji wa misituni.
Joseph Kabila amekuwa turufu ya kisiass Kongo Kinshasa. Ni yeye, Joseph Kabila aliyeikuta nchi imegawanyika vipande vipande na kuweza kuiunganisha kwa kiasi kikubwa.
Ni Joseph Kabila zao la mfumo wa kiintelijensia ya kijeshi ya Tanzania.
Ni kutokana na sababu za kihistoria na jiografia ya kisiasa ( Geopolitics), Tanzania mara zote imehakikisha inabaki na ushawishi kwa yanayotokea Kongo- Kinshasa.
Na kimsingi, Joseph Kabila bado yupo katika mfumo wa utawala wa Kongo.
Historia ni Mwalimu Mzuri. Laurent Kabila ( Pichani kulia) aliingia Mashariki ya Kongo na karata mbili, ya kwake na ya mwanawe. Alijaribu kufanya hivyo miaka ya 60 akisaidiwa na Che - Guevara. Alishindwa.
Kwanini?
Jibu lake ni simulizi nyingine.
Vinginevyo, mradi mkubwa wa ' Kabila dynasty' ni kujenga ' Democratic Republic of Congo- DRC'.
Ieleweke hapa, kuwa inapohusu Kongo- Kinshasa, tunazungumzia himaya tatu zenye kugombea kutoa mtawala:
BaAlunda, BaAluba na BaHima. Mashariki ya Congo wapo WaAluba. BaHima pia wapo bila kusahahau himaya nyingine ndogo ya Bayeke.
Banyamulenge wale walitokea kwenye BaHima. Kagame na Museveni wana asili ya BaHima. Kumbuka watu wa aina ya Sultan Makange na Laurent Nkunda. Kumbuka pia M23.
Tanzania tulikwenda DRC na vikosi vyetu kuwamaliza M23 kwa vile walitishia maslahi yetu. Kihistoria Wa- BaAluba ni wenzetu.
Na marehemu Nkurunziza anapoandamwa na wenye asili ya Himaya ya BaHima Tanzania kwa namna moja au nyingine ilichagua upande.
Suala la Kongo- Kinshasa ni gumu lakini linafafanulika. WaAlunda wenye Kinshasa yao wanaongea Kilingala na wanakizungumza Kifaransa cha wakoloni wao.
Kumbuka, Kabila baba alipouawa, watu wa Kinshasa hawakumpokea vizuri mwanawe Joseph Kabila. Mitaani Kinshasa walisema kuwa, Joseph hajui kuongea Kifaransa. Akawashangaza siku ya kuapishwa kwake alivyozungumza Kifaransa.
Siri yake?
Laurent Kabila alihakikisha anamwandaa Joseph siku itakapofika kwenda tena Kongo- Kinshasa na hususan kupitia Mashariki ya Kongo.
Ni kwenye kukamilisha mpango wa tangu enzi za baada ya kuuawa Lumumba. Mpango wa kuirudisha Kongo tena, na mara ya pili kwa kuijenga inayoitwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo. Kwamba Kongo mpya haitakuwa ya WaAluba tu, ni ya wote.
Ikumbukwe, Laurent Kabila alikuwa mfuasi wa Lumumba. Alikuwa Mjamaa ambaye kukimbilia kwake Tanzania baada ya Lumumba kuuawa mwaka 1961, ilikuwa ni jambo lililotarajiwa.
Joseph Kabila amezaliwa kwenye ardhi ya Tanzania. Ni kizazi cha tatu cha Kongo ya Lumumba. Amekulia Tanzania pia, lakini, Laurent Kabila alikuwa akimwandaa mwanawe kwa ' Wimbi la pili' la Mapinduzi ya Kongo.
Joseph Kabila mitaani na shuleni alikopitia Tanzania amekuwa akiongea Kiswahili kama Waswahili wengine, lakini, kwenye familia ya Laurent Kabila, nyumbani pale Kunduchi Mtongani, kimkakati, kiliongewa Kifaransa.
Ndio maana watu wa Kinshasa walishangazwa mwaka ule 2001 kumwona Joseph aliyezaliwa na kukulia Tanzania siku ya kuapishwa aliongea Kifaransa.
Laurent Kabila kwenye kumwandaa mwanawe Joseph Kabila alihakikisha anapitia mafunzo ya kijeshi pia.
Ukiacha JKT ya Tanzania ambayo ilikuwa ni kwa mujibu wa sheria, wakati Laurent Kabila na wenzake wakijiandaa na wimbi la pili la kuingia Kongo, Joseph Kabila alipata mafunzo zaidi ya kijeshi. Alimpeleka mpaka Uchina pia kupata mafunzo ya kijeshi.
Ni Tafakuri Jadidi.
Maggid Mjengwa.
Dar es Salaam.