Mla Bata
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 7,841
- 17,491
Wasalaam,
Appease, Propitiate and Placate!
Tuliza, Fidia, wape waone na kusikia wanachotaka kusikia!
Kwenye sayansi ya siasa hizi ni nguzo zitumikazo mara kwa mara kuongoza, ebu leo tujikite kwenye Placate.
Placate (play-cat), it's a mind game, una control akili za watu kwa kuwaonyesha wanachotaka kukiona na kuwasikilizisha wanachotaka kusikia kwa muda husika ili upate ama kupoteza attention,focus yao/zao kwenye jambo fulani, zingatia hayo maneno mawili, UPATE ama KUPOTEZA focus/ attention zao.
Kwa maana gani?
Placate hutumika kujenga ama kubomoa, kinachotokea sahizi kwenye nchi yetu ni Placate, Watawala wana "play-cat", wanajua wananchi wake hasa kundi fulani lililo kwenye mitandao ya kijamii ( X/Twitter mathalani) wanataka nini, mihemko yao ipo kwenye mambo gani?
Wanatuonyesha au kutusikilizisha jambo fulani Zuri au baya (mara nyingi ni baya) ili waweze kupata attention zetu (mara zote wamefanikiwa katika hilo), huku lengo lao likiwa kupoteza focus na attention kwenye jambo lingine.
Kwenye uwanja wa mpira wa miguu mara zote aliye nje ya uwanja huweza kuona vizuri zaidi kinachoendelea kuliko aliye ndani ya ground. Mtiririko wa matukio yanaoendelea kipindi hiki kwa haraka haraka unaweza kudhani yanatokea kwa bahati mbaya, la hasha, it's a mind game, and they got us right.
Alitekwa yule kijana afisa Ubashiri wa X, attention yote ikahamia hapo, kelele zote na lawama kwa mamlaka zikashika hatamu, ghafla watoto pendwa wa familia wakafukuzwa nyumbani, was that a coincidence???
Image ya jeshi letu la ulinzi na usalama ikachafuliwa na wahuni 5/6 kwa weredi wao huku wakidai "mtoto kautaka mwenyewe" wizara husika na serikali ikaingia matopeni tena. Habari ya mjini mitandaoni ikawa ndio hio, kuanzia mawakili waandamizi mpaka wanaharakati nguli tukajikuta tumesahau yale yaliyokwisha kutokea nyuma.
Punde si punde Viongozi wa Chadema wote wakakamatwa pamoja na gen z wao, kwa muda tukasahau wale baradhuli watano na akili yote imehamia kwa makamanda, jioni tunamsikia kiongozi mmoja akimuamulu waziri husika awaachie makamanda na gen z wao inafikirisha, wataachiwa, je tutarudi kwenye lipi Sasa? Wait nakumbushwa hapa yule kijana aliyechoma picha ya mkuu, kukamatwa, kuhukumiwa na kuachiwa Kisha kupotezwa hajapatikana bado, vipi tutaanza na hilo?
Hii ni miluzi mingi yenye malengo ya kumpoteza mbwa muindaji, natamani kuona siku upinzani ukistick na kufocus kwenye agenda zake muhimu ilizojiwekea.
Maswali ya msingi, ni kweli Watawala wamefanikiwa kucheza na akili zetu, ni kweli watawala wanaweza kuamua tuwaze nini na kuzungumza jambo gani na wakati gani?
Kama ni kweli, Je hizi siasa za mihemko na kufuata "trends" za mitandao zitawafikisha wapinzani nchi ya ahadi?
Wasalaam.
"Everything is possible for those who believe" lets meet at the top, cheers 🥂.
Mla bata
München, Deutschland 🇩🇪.