Tafakuri: Je, wasanii Watanzania wanaipenda CCM au ni njaa inawasumbua?

Tafakuri: Je, wasanii Watanzania wanaipenda CCM au ni njaa inawasumbua?

Pesa za mabeberu wale CDM, kuimba waje kuimba wasanii wa Tz...
Mwambie Lissu alete wasanii wa Kenya, yeye si ana damu ya Kenya 🤣
 
Dah...Mrembo...Kuna wakati tuweke ujinga pembeni ili tufikiri kwa uhuru.....wote hawa Magufuli, Lissu, Mzee wa ubeche na kuku, Membe njaa ni sababu mojawapo inayofanya wagombee....Kulialia kwa Lema na Gambo wote ni sababu ya njaa...Madongo kati ya msagaji na yule mcheza sinema eksi yote ni sababu ya njaa.

Ni bodaboda mpumbavu tu atakayekataa kukodiwa CDM eti tu ni mfuasi wa CCM

Ni fundi ujenzi mjinga tu atakayekataa tenda ya ujenzi kutoka CCM eti tu kwa sababu ni mfuasi wa CHADEMA..... Hata wewe utakuwa mjinga kama ukikataa tenda ya kugawa vinywaji kwenye mkutano wa CCM.....kila mmoja anapambana na njaa yake kwa namna yake....Sitashangaa kama njaa yako ndiyo imekusukuma kuleta uzi huu...... 😎
 
Sio kwamba madhila yanayoendelea hawayafahamu hapana wanafahamu sana tena sana, ila ngoja nikung'ate sikio, aneogopwa ni mungu wa Chattle kwake yeye kila pambio litaimbwa. Sasa ukijumlisha uoga na njaa jibu lake unafiki wa kiwango cha tuta la SGR.
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wasalaam,

Kuna mambo mengine yanahitaji kufikiri kwa upana hasa kipindi hiki tunapoelelea katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Nimefatilia uzinduzi wa kampeni za CCM pale uwanja wa Jamhuri Dodoma, nimeangalia nyuso za wasanii waliotumbuiza katika tamasha lile la CCM na kuona wengi wana mashaka katika kile wanachoimba. Nimeshindwa kutambua yale ni mahaba kwa CCM, njaa, au bendera fata upepo?

Wasanii wa bongo wamekuwa wakitumika na CCM kila unapofika Uchaguzi na baada ya Uchaguzi wamekuwa wakitupwa katika dustbin kama takataka nyingine zitupavyo. Hivi ni kweli wasanii hawa hawajitambui au ni njaa inawasumbua? Hivi ni kweli wasanii hawa hawaoni Uhuru wa vyombo vya habari ulivyoyumba? Hivi ni kweli wasanii hawa wamesahau yaliyowakumba katika miaka5 ya CCM? Maana kuna waliotekwa, kufungiwa nyimbo zao n.k hawayakumbuki haya au wametishwa?

Mwisho nawakumbusha wasanii wekeni maneno yangu akiba baada ya Uchaguzi kwisha CCM hao hao watawasomesha namba, CCM ni ile ile haijawahi kumtetea mnyonge.

Maendeleo yana vyama.

Nukuu ya leo "Siwezi kupeleka maendeleo jimbo mlilomchagua mpinzani". (Kauli ya Rais Magufuli akiwa Lindi)
Njaaa hata Diamond anayejifanyaga ana pesa ameshikwa na njaa.
 
Daa
Bora waende CCM penye uhakika,kwanza wapinzani ni blabla nyingi tu, mnampigania mtu mpaka mnaumizwa na polisi mwisho wa siku anakwenda CCM.
Daah nasikia walipewa rushwa ya pesa na vyeo si unajua rushwa na ccm ni sawa na uji na mgonjwa
 
Wale ni kama daladala unaweza kupeleka utakako ilimradi umlipe
 
Daa

Daah nasikia walipewa rushwa ya pesa na vyeo si unajua rushwa na ccm ni sawa na uji na mgonjwa
Rushwa zipo tu mbona,Chadema kuna rushwa mpaka za ngono kwa viti maalum.
Lowasa alimuhonga pesa ndefu Mbowe ili apewe nafasi ya kugombea urais ndani ya Chadema.
 
Back
Top Bottom