njasulu
New Member
- Jul 18, 2022
- 4
- 8
Mara nyingi nimekuwa nikitafakari, ni namna gani nimefika hapa nilipo. Siku zote naona ni kama kitendawili kwa maana ni mambo mengi yanahusika hadi mtu kufikia hatua yoyote katika maisha yake, iwe ni kupata kazi, kupata mtoto wa kwanza, kumzawadia mtu wake wa thamani ili apate furaha ndani yake lakini pia hata majonzi, kupata ajali, kufukuzwa kazini nakadhalika.
Kama binadamu ni machache tunaweza kuyadhibiti, mengi ya hayo hatuna nguvu juu yake maana tumejikuta kwenye mfumo wa maisha ambayo tumefundishwa na watu tulikuwakuta kabla yetu.
Tumefundishwa kuheshimu waliotuzidi kwa rika tangia udogo wetu kutoka kwa wazazi na walezi. Lakini katika kukua kwangu, ninashuhudia mabadiliko ambayo yanachukua nafasi kubwa katika familia zetu za sasa, hakuhitajiki tena mtu kumzidi mwingine ili aheshimike, tumeona kuna kiungo kipya kwenye jamii zetu kinachotafsiriwa kama uwezo na hasa wa kifedha ndio ninalo huisha hapa.
Turudi nyuma kidogo kutambua ni wapi hili badiliko lilitujia.
Sisi kama taifa na kwa uwepo wa jamii zetu za jadi ambazo zimekuwa zikitawala ardhi hizi kwa mamia ya miaka na mifumo iliyokuwa ikifanya kazi kabla badiliko hili halijatukumba.
Wengi wetu tumekuwa tukikana uhalisia wetu, machimbuko yetu kama waafrika, na si kosa letu kizazi cha leo, wala si kosa na kizazi cha wakati huo ambapo badiliko hili lilipoanzia, si ujinga wala upumbavu wa vizazi vilivyotupita, mtazamo wangu unasema ni ukarimu wetu uliopindukia kwa wageni ambao walikuja kwetu kuomba hifadhi.
Jamii zetu zimekuwa zikiishia kwa namna yake ya kipekee, ambayo wengi wetu tumepumbazwa na kuacha kuifatilia tena, tumekuwa tukipewa historia yetu na mwandishi ambae si wa nyumba yetu, kwanini? Tumekubali kuingia kwenye madarasa kujifunza historia ya mgeni wetu na kutukuza yale yote aliyoyatenda kwa wema na ubaya juu yetu huku akitupa fundisho la uduni wa hali zetu, mila zetu, imani zetu, jinsi yetu ya kuishi kwanini?
Kwanini tunaamini namna yake ya maisha ndio bora kuliko yetu? Tukaamua kukumbatia yale yote tuliyoletewa na mgeni huyu? Kwanini tumepoteza uasili wetu, uafrika wetu?
Tamaduni zetu zinaonesha tangia kipindi cha mwanzo kabisa, baba amekuwa ndio kichwa cha familia na mama akiwa kiungo pekee cha kuitunza familia. Hakujawahi kuwa na shida yoyote katika familia zetu kuendana na mfumo huo. Katika baadhi ya makabila nchini kwetu kuna jamii ambazo zinaongozwa na wanawake kama kiongozi wa familia, ingawa changamoto zimeumbiwa mwanadamu tunashudia uimara wa jamii hizi chache katika namna yake ya kipekee. Kwanini leo hii tumetokea kukandamiza haki na weledi wa mama zetu ambao sambamba nao tulishirikiana kufikisha jahazi la uhalisia wetu hadi pale mgeni alipotuingilia.
Inawezekana vipi tufundishwe ujio wa binadamu kama masokwe wakitokea Afrika lakini hatuambiwi yale makubwa yaliyotokana na watu wa Afrika na mchango wetu katika kuifikisha dunia hadi hapa ilipo? Kwanini tamthilia na majarida ya kidini ya kikristo zinatolea mfano wa mesia akiwa ni wa asili ya mgeni wetu ilhali chimbuko la historia nzima ya dini ya kikristo inatokea bara la asia ya magharibi? Kuna kitu gani kinafichwa hapo?
Tumefundishwa makuu yaliyotendwa na falme kubwa ulaya, ambao walifikia kutawala hadi mbili ya tatu ya dunia lakini hatukokaa kusikia historia ya wana wa asili ya Moors wakitokea Afrika na asia wakifkia na kuweka tawala zao barani ulaya kwa miaka zaidi ya 600, wakijenga mahekalu na majumba ya kifahari na kuleta usasa wa majengo uonaoonekana katika nchi ya hispania.
Mahekalu na masinagogi yanayoonekana nchi ya Ethiopia ambayo yamekuwepo kabla ya falme zote za Ulaya hayaongelewi mashuleni mwetu inavyopaswa. Utajiri ulionekana na wageni wa kwanza walipofika kwenye fukwe za Afrika magharibi na kuwastaajabisha kwa utajiri wa dhahabu, ukubwa wa biashara ulifikiwa kati ya Afrika Magharibi na Asia ya kati, upana wa mahekalu yaliyojegwa katika falme za Sonhgai, Ono, na Mali. Wangapi wanafahamu chuo kikuu cha kwanza kabisa duniani, kutengenezwa Afrika ya magharibi, kilichokua na maktaba kubwa duniani kwa wakati wake na tafiti mbali mbali ambazo aidha zilinyang’anywa au kuteketezwa na mgeni alivyokuja kukamilisha lengo lake?
Je, tunajifunza kutoka jamii zingine ambazo zinaonekana kukinzana na tamaduni ambazo zimewekwa na wageni wetu? Je, tunaangalia ni namna gani na wao wameweza kuwashinda kwenye mchezo wao wenyewe? Ni lini tunaweza kuona ya kwamba msaada wetu kutoka katika umaskini huu tulioletewa na mifumo duni kutoka ulaya, mifumo kandamizi ambayo inayonya si rasilimali zetu bali nguvu kazi ni sisi wenyewe?
Miaka ya 1900 China walianza mapinduzi yao kujikwamua kitamaduni, wakipigana vita vya wenyewe kwa wenyewe wakijua wanachopigania si uhuru wao kama watu ambao hawataki kutawaliwa lakini pia wakipinga nguvu ya tamaduni kutoka mataifa mengine. Imekuwa kama bahati kwao, kwa utambuzi huo mapema ndicho kinachoonekana leo, kuwa ni taifa kubwa lenye nguvu duniani kote. Huu ni mfano mmoja tu, ipo mifano mingi sana ya hivi karibuni ikiwemo muunganiko wa nchi za kiarabu.
Dhumuni la andiko hili fupi si kuhadithia historia, bali kuonesha ya kwamba uamuzi ni wetu sisi kama vijana wa kizazi kinachotarajia kuiona kesho. Ni dunia yetu kwa pamoja tunatakiwa kuijenga kwa ajili ya vizazi vijavyo. Nia yangu ni kupandikiza mbegu ya tafakuri hii kwako, tuwaze pamoja na kuchanganua ni mambo gani ambayo yanawezekana kufanyika kutoka kwetu ili vizazi vijavyo viweze kujikwamua na wimbi la umaskini na utumwa wa kifikra unaotukumba. Tuamue kufufua tamaduni zetu, tujifunze kuuliza maswali na kuchanganua majibu kwa manufaa yetu kama taifa.

Upvote
5