Tafakuri: Mwisho wa wiki, Mwisho wa mwaka 2022

Tafakuri: Mwisho wa wiki, Mwisho wa mwaka 2022

masopakyindi

Platinum Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
18,207
Reaction score
13,839
Kabla sijalala usiku huu nimeingiwa na tafakari nzito.

Leo tayari ni 31st Dec 2022, siku ya mwisho wa mwaka 2022.

Namshukuru Mungu kwa kunipa ingalau kuiona hii siku.

Rafiki yangu, tena wa cheo cha juu, alifariki SIKU YA KRISMASI! Na tumempumzisha jana.

Mimi nimempa nini Mungu?
Ni rehema zake tu
Wana JF, pamoja na mabishano mengi humu mtandaoni, siku hii ni ya kumshukuru Mungu, kila mtu kwa dini yake.

Kesho jumapili ni tarehe 1 mwezi Januari 2023.

Bado hatujaiona, tumwombe Mungu tuifikie maana si wote wataiona siku hiyo.

Tena tukijaaliwa ,tutauona mwaka 2023 kwa kuanzia siku ya kumwomba, kusifu na kumshukuru Mungu, tarehe 1 January 2023, siku ya jumapili!

Tarehe hizi na nyakati hizi ni muujiza mtupu, tumshukuru Mungu.
 
Ameen.

Tumshukuru Mungu Kwa kila Jambo. Pumzi na uhai ni vya kwake.

Happy new year in advance to all
 
Better still, ni mwisho wawiki, mwisho wa mwezi, mwisho wa mwaka!
 
Back
Top Bottom