PreGE2025 Tafakuri ya kisiasa na kijasusi; Majibu ya kitoto kwa hoja nzito za Askofu Gwajima

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

TJF1990

Member
Joined
Nov 1, 2023
Posts
6
Reaction score
17
Na: Mwananchi Mzalendo
Tarehe: 27 Mei 2025

Siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita (24 May 2025), Askofu Josephat Gwajima—Mbunge wa Kawe na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM—alizungumza na waandishi wa habari na kutoa kauli nzito juu ya matukio ya utekaji yanayoendelea kushamiri nchini. Kwa maudhui na uzito wa kauli yake, hii haikuwa tu hotuba ya kawaida ya kisiasa, bali ni signal ya kiintelijensia inayofaa kuchukuliwa kwa umakini wa hali ya juu.

Nikiwa kada wa CCM wa muda mrefu na mstaafu wa taasisi nyeti za dola, niliwahi kuwa miongoni mwa waliompinga Gwajima asiwe mbunge. Lakini kwa uaminifu wa kiakili na kimaadili, ninakiri hadharani: nilikosea. Tangu awe mbunge, Askofu Gwajima ameonyesha ukomavu, uthubutu na msimamo wa nadra sana katika siasa za Tanzania. Sauti yake si ya fujo, bali ya ujasiri wa anayejua hatari ya kukaa kimya wakati ukweli unateseka.

1. MBINU ZA KUZIBA HOJA KWA KELELE

Baada ya kauli ya Gwajima, tumeshuhudia baadhi ya watu wanaoonekana kutumwa na wenye mamlaka wakiwa majibu yenye muundo wa reactionary propaganda badala ya hoja za msingi. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba wanaojaribu kumjibu Askofu Gwajima si watu wenye weledi wa hoja, bali vijana na wanaharakati wa mtandaoni waliopewa jukumu la kumdhibiti kwa matusi au kejeli. Hii ni mbinu ya kijasusi inayoitwa distraction by ridicule—kugeuza mjadala mkubwa kuwa mzaha ili kuua nguvu ya hoja. Kwa mtu wa aina ya askofu Gwajima ni vigumu kutumia mbinu hii kwenye hoja zake na kushinda.

Pia soma: Pre GE2025 - Askofu Gwajima: Wakuu wa Vyombo vya Usalama wasiondolewe kwenye nafasi zao kwa mapenzi ya mwanasiasa aliyewaweka

Kwa mfano, siku ya jana, Jerry Muro aliandaliwa press conference ili kumjibu Askofu Gwajima. Ni wazi kuwa Jerry Muro hana uwezo wala sababu ya kutumia fedha zake kuwaita waandishi wa habari na kuongea nao. Ni dhahiri kuwa alitumwa na baadhi ya wakubwa kuwasemea. Hata hivyo kwa sababu ya uwezo duni alionao wa kujenga hoja alitumia fursa hiyo kuishushia hadhi ofisi ya Rais aliyokusudia kumtetea. Press conference ya Jerry Muro ilikuwa ni utani uliopitiliza kwenye hoja ya msingi. Matusi na maneno ya kebehi aliyoshushiwa na udhibitisho usio na shaka kuwa ni heri angekaa kimya kuliko kuongea alichoongea. ALIHARIBU SANA KILE ALICHOKUWA ANAJARIBU KUKIJENGA.

Leo pia nimewaona baadhi ya vijana na viongozi wa UVCCM wa jimbo la Kawe waliondaliwa press conference kumjibu askofu Gwajima. Kwa kweli nimesikitishwa sana na press conference hiyo. Inaonekana kuna ombwe kubwa sana la uongozi ndani ya CCM na taasisi zetu nyeti. Yule aliyewatuma vijana hawa inatakiwa achukuliwe hatua za kinidhamu za kudhalilisha chama. Majibu ya vijana hawa yamezidisha hasira za umma badala ya kupunguza. Mambo kama haya yaliyofanywa na hawa vijana ndiyo hufanya CCM idharauliwe. Mambo ya kijinga kama haya ni muhimu sana yadhibitiwe ili kulinda hadhi ya CCM na taifa letu.

2. ASKOFU GWAJIMA HAJAANZA LEO KUKOSOA NA KUTOA MAONI BINAFSI KWENYE MAMBO YA KITAIFA

Askofu Gwajima hajaanza jana kukosoa au kutoa maoni binafsi juu ya mambo ya kitaifa. Mtakumbuka kuwa wakati wa Rais Kikwete, Askofu Gwajima alizungumza kuhusu kutekwa kwa Ulimboka. Kipindi cha utawala wa rais Magufuli, askofu Gwajima alikemea jaribio la mauaji ya Tundu Lissu, utekaji wa Roma Mkatoliki, na kutoweka kwa Ben Saanane. Sasa, chini ya Rais Samia, bado askofu Gwajima anazungumza. Suala la askofu Gwajima ni msimamo wa kimaadili unaovuka awamu za uongozi. Kwa muda niliomfatilia Askofu Gwajima kwa hoja zake, nimegundua kuwa si mtu wa kutumika, bali mtu wa kusimamia dhamiri.

Jana, nimewasikia baadhi ya wabunge jana na wao wakifanya propaganda dhaifu juu ya hoja za askofu Gwajima. Kosa kubwa linalofanywa na washauri wa kisiasa wa serikali ni kufikiri kuwa Askofu Gwajima ni tishio kwa Rais Samia. Ukweli ni kwamba, hoja ya Gwajima ni tishio kwa mfumo usioheshimu utu wa binadamu na usalama wa raia—siyo tishio kwa taasisi ya urais yenye dhamira safi.

3. HOJA SI MTU—HOJA IJIBIWE KWA HOJA

Kwa mujibu wa kanuni za counterintelligence, hoja kama hizi za Askofu Gwajima zinapaswa kuchambuliwa na kushughulikiwa kwa kutumia strategic communication and de-escalation protocols. Kutoa majibu ya hasira au ya kutilia shaka tabia ya Gwajima binafsi ni ushahidi wa kufilisika kwa hoja.

Kusema kweli hadi sasa, hakuna mtu aliyetoa majibu ya msingi kwa hoja alizozitoa. Badala yake, tumeshuhudia watu wakihamishia mjadala kwa mtu badala ya ujumbe. Hii ni mbinu ya kisiasa inayoshindwa mara zote dhidi ya wapinzani wenye misingi.

4. MAJIBU HAYA YA KITOTO YANAATHIRI TAASISI ZA DOLA

Wakati watu wanapotumwa kumshambulia Askofu Gwajima kama mtu, wanazidi kuonyesha kuwa hoja zake ni sahihi kwa sababu zinawatia hofu. Na zaidi ya hapo, wanachofanya si kumshambulia Gwajima pekee, bali wanadhoofisha sura ya serikali na taasisi zake mbele ya wananchi. Kitaalamu, hii inaitwa blowback effect—yaani, propaganda inarudi kuharibu anayeitumia.

Mtu hawi hatari kwa sababu ya kusema tofauti. Hatari hutokea pale mfumo unashindwa kujibu hoja kwa hoja, bali unataka kuua sauti ili kulinda picha. Ni kupitia mvutano wa hoja ndipo nuru ya ukweli hujitokeza. Kwa hiyo, kauli ya Gwajima—hata kama ina hisia au msisimko—haipaswi kupuuzwa kama “narrative ya kisiasa”, bali kuchukuliwa kama mchango katika kutafuta ukweli wa taifa.

Majibu haya ya kitoto juu ya hoja nyeti ya Gwajima yanajaribu kuonyesha kuwa askofu Gwajima ana ajenda yake ya kisiasa ndiyo maana anaongea anachoongea. Watu hawa huenda hawajui kuwa askofu Gwajima amekuwa akitoa hoja za namna hii hata kipindi hajawa mwanasiasa. Jamii inayodhani kila kauli ni mpango wa siri, huzaa kizazi cha watu waoga, waliopoteza dira ya maadili ya kweli. Hii ni hatari kuliko hoja yoyote ya kisiasa.

HITIMISHO:

Askofu Gwajima ana hoja. Hahitaji makofi wala shangwe. Lakini anahitaji majibu ya hoja, si mashambulizi ya binafsi. Kwa wenye mamlaka, ni busara kujifunza kwamba si kila anayekosoa ni adui. Wakati mwingine, anayesema ukweli mchungu ndiye rafiki wa kweli wa taifa.

Si kila anayesema ukweli wa maumivu ni tishio la usalama. Kukosoa taasisi ya urais si uhaini, ni kiashiria cha jamii inayojitambua. Kumsikiliza Gwajima si lazima kuafiki, lakini ni ishara ya demokrasia hai. Jamii inayoogopa sauti tofauti hujenga ukimya unaoza.

Kwa wale wanaotumia “watoto wa kisiasa” kumjibu Gwajima: tambueni kwamba hoja kubwa haziwezi kufunikwa na kelele ndogo.

Ukiniuliza mimi kati ya Gwajima na hawa wanaojaribu kumjibu Gwajima; ni Gwajima anamsaidia Rais. Hawa wengine wanaojipendekeza kwa majibu ya jaziba hawampendi Rais. Wanajipendekeza kwa maslahi binafsi. Wanataka kumtumia Rais kufanikisha njaa zao.

Mwananchi Mzalendo
27 Mei 2025
 
Akili kubwa sana
 
Kitu kimekaa vizuri kabisa, nimependa. Gwajima kwa hoja zake ni msaada mkubwa sana kwa Taasisi ya Urais wa JMT na Wanzania kwa ujumla wake kuliko hao wanaojipendezekeza kwa ajili ya kutafuta maslahi yao binafsi na mwisho wa siku wanayoyaongea yanaendelea kusababisha gap kukua kati ya Raia wa JMT na serikali yao iliyopo madarakani yenye wajibu wa kulinda raia na mali zao, lakini sasa Raia ndio hao kila kukicha orodha ya wanaopotea inazidi kuwongezeka na hakuna majibu zaidi ya kejeli za akina Jerry Muro
 
Upembuzi yakinifu, cha kusikitisha ni kuwa ukweli wanaujua ila wanapuuzia kwa makusudi kulinda mambo yao, hoja ya uzalendo ni unafki.
 
Back
Top Bottom