Elections 2010 Tafakuri ya mkutano wa JK Lindi!

Elections 2010 Tafakuri ya mkutano wa JK Lindi!

Deodat

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2008
Posts
1,274
Reaction score
274
Tathmini ya watu waliohudhuria mkutano wa Jk, jionee mwenyewe kwenye picha.

Picha kwa hisani ya KZ.
 
Attachments

  • 67678_452824340137_772270137_5232422_7060966_n[1].jpg
    67678_452824340137_772270137_5232422_7060966_n[1].jpg
    69.3 KB · Views: 216
watu wanafuata fiesta....hahaaa Tzama mikutano ya Dr.Slaa watu wanatamani wangeenda na note book wawe wanachukua notes
 
Tofauti ya hii mikutano ni mikubwa kiwete anajaza akina mama na watoto slaa mikutano yake inahudhuriwa na wanaume na vijana! Hata ukitazama kwa umakini hata hamasa ya watazamaji! Kikwete hujaza watu ingawa watu hawana hamasa kusikia au kushangili kwa slaa ni kinyume chake!
Huu ni utofauti unaonekana ukichunguza kwa umakini na kuacha wanachokizungumza
 
ANGALIZO TU MKUU HAPO PENYE RED:
Akina mama ndiyo base kubwa ya JK na ndiyo maana pengine watampa ushindi, kwani wao (akina mama) mara nyingi hu-vote from their hearts, and NOT from their heads. Sura ya JK huwa inawagalagaza wanawake wengi na kama umeaona utitiri wa mabango, ni picha ile ile ya JK (nadhani ya late 90s).

Fikiria: Kama mtu angekuwa na uwezo siku ya kupiga kura kuwazuia nusu ya wanawake nchini wasiende vituoni kupiga kura, basi CCM (na hasa JK) itakuwa taabani! I think you know what I mean!
 
Duh,nime kubali analysis hiyo,uko makini sana
 
Chadema lazima ijihadhari na kura za kinamama kwani wao ndio hasa husababisha ushindi ktk tawala nyingi (wapigakura)...Kazi kwenu!
 
Kafiri bangi&mkandara mliyosema kweli tupu nimeona hata nguvu ya maalim seif ukiangalia akina mama ni wengi kushinda wanaume! Kweli hawa ndio wanaopiga kura tatizo lao ni conservative mno! Ndio maana hata mama wa kwanza kashangaa imekuwaje akinamama wa mkoani mby (tunduma) kumuonesha alama ya v!
Mtu anayeweza kuteka akina mama ana additional advantage kwani hawabadiliki kirahisi pia wana njia nyingi ya kujikusanya katika vikundi kama vya kuweka na kukopa, kufa na kuzikana hata upatu!
Urahisi wao kuungana unamaanisha kuna mtu wanamuamini kama kiongozi wao huyu huwa na ushawishi mkubwa akisema lolote huaminika na wenzie kuwa ni kweli!
Viongozi walio madarakani hasa madiwani hujitahidi kuwa jirani na viongozi wa vikundi hivyo (nifae kwa masika nikufae kwa kiangazi) kipindi kama hiki hutumika sana,kama ni fungu huyu hupewa yeye akawashawishi wenzie hapo ndipo kazi ilipo kumbadili mwanamke ambaye kaambiwa na mwanamke mwenzake habari haijalishi kweli au uongo na akasisitiziwa kabisa wanaume sio watu wa kuwaamini kazi ipo! Ila tujipe moyo sio kweli kuwa wanawake wote wapo chama kimoja hata kama upande mmoja una wanawake wengi ila na upande wapili upo!!
 
Chadema lazima ijihadhari na kura za kinamama kwani wao ndio hasa husababisha ushindi ktk tawala nyingi (wapigakura)...Kazi kwenu!

Ni kweli, akina mama ndio ambao huwa na 'turn out' kubwa wakati wa kupiga kura, sie akina baba tukijifanya busy. Ndo hapo sisiemu inapoibuka na ushindi wa kishindo.
 
Ni kweli, akina mama ndio ambao huwa na 'turn out' kubwa wakati wa kupiga kura, sie akina baba tukijifanya busy. Ndo hapo sisiemu inapoibuka na ushindi wa kishindo.

Idimi you are right, suala la kujitokeza kwa wingi this time is imperative.

VOTE FOR CHADEMA
 
Waulizeni Mara, akina mama wanaambiwa kama unaenda kuichagua ccm bora ukae chumbani siku ya uchaguzi. Wanaume ndo wanahalalisha hiyo hali ya akina mama kuichagua ccm.
 
ANGALIZO TU MKUU HAPO PENYE RED:
Akina mama ndiyo base kubwa ya JK na ndiyo maana pengine watampa ushindi, kwani wao (akina mama) mara nyingi hu-vote from their hearts, and NOT from their heads. Sura ya JK huwa inawagalagaza wanawake wengi na kama umeaona utitiri wa mabango, ni picha ile ile ya JK (nadhani ya late 90s).

Fikiria: Kama mtu angekuwa na uwezo siku ya kupiga kura kuwazuia nusu ya wanawake nchini wasiende vituoni kupiga kura, basi CCM (na hasa JK) itakuwa taabani! I think you know what I mean!

Kwa hiyo mama yako na dada yako they vote from their hearts sio? Ofkoz kama Chadema mngekuwa serious mngefanya breakdown ya voter demographics and make an attempt to appeal to women. Now, mnamcheka Mama Salma akizunguka nchi nzima. Unadhani kura za kina mama zitashuka toka mbinguni kwa sababu Kakobe au Padre Slaa walikuwa watu wa Kanisa?

Hamko serious--
 
ANGALIZO TU MKUU HAPO PENYE RED:
Akina mama ndiyo base kubwa ya JK na ndiyo maana pengine watampa ushindi, kwani wao (akina mama) mara nyingi hu-vote from their hearts, and NOT from their heads. Sura ya JK huwa inawagalagaza wanawake wengi na kama umeaona utitiri wa mabango, ni picha ile ile ya JK (nadhani ya late 90s).

Fikiria: Kama mtu angekuwa na uwezo siku ya kupiga kura kuwazuia nusu ya wanawake nchini wasiende vituoni kupiga kura, basi CCM (na hasa JK) itakuwa taabani! I think you know what I mean!

Good analysis, midume mingi ipo busy for nothing na haitapiga kura au itaenda vituoni imechelewa - huo ndiyo ukweli
 
Lakini uhafidhina (conservatism) wa akina mama una limits. Kama nilivyosema, hu-vote from their hearts and not from their heads. Hii ina maana mara nyingi hawachambui sana sifa za mgombea na uwezo wake, bali anaukwa carried na masuala mengine kama vile appearance n.k. Mimi naamini kabisa wengi wa wale wanawake ambao ni educated enough hawana uhafidhina ninaosema.

Isitoshe akina mama wenyewe kwa wenyewe hawajipendi -- yaani katika kuwaona wenzao wakigombea. Wako tayari kumchagua male candidate kuliko female mwenzao. Tumeona hivyo katika uchaguzi wa Marekani mwaka 2008. Wanawake wengi weupe (katika Democrats) waliamua kumpgia kura Obama kulko Hillary Clinton mweupe mwenzao. In fact Wamarekani (ambao kama kwa nchi nyingine nyingi tu) idadi ya wanawake ni kubwa kuliko ya wanaume waliona ni bora kuwa na rais mwanaume, ingawaje ni black, kuliko mwanamke ambaye ni white. Usisahau Blacks make only 30 % of US population.
 
Back
Top Bottom