Tafiti inasema Binadamu huwa na wastani wa Kukoswa na Kifo Mara Sita, Mimi zimebaki Tatu!, wewe je?

Tafiti inasema Binadamu huwa na wastani wa Kukoswa na Kifo Mara Sita, Mimi zimebaki Tatu!, wewe je?

Ikiwa ni Usiku Mwingine Tulivu tena, wanaJF niwakaribisheni katika Uzi huu Maridhawa wa Kushirikishana tafakuri mbalimbali za Maisha..
Leo tuangalie hii case ya Changamoto ya Kukoswa koswa na Kifo, Either kwa Ajali au Hata Ugonjwa
Kuna tafiti inayosema kuwa binadamu ana wastani wa kukoswa na kifo Mara sita, yaani kunusurika na Kifo Mara sita kwa wastani.

KWA MIMI HAPA!

Mama yangu ananiambia sikuwa mtu wa kuumwa mara kwa mara.. naweza kumaliza hata Miaka miwili bila kuguswa hata na Mafua, Anasema mwaka 1998 nilipigwa na Malaria moja hatari sana.. Mama anasema alijua nimekufa.. Alilia sana.. Hata wakati Madaktari wanamwambia niko hai "Hakuamini"

Mara ya Pili ilikuwa October 2005, Nilikuwa Darasa la Nne, nakumbuka ilikuwa kipindi fulani cha kupatwa kwa mwezi.. Nilipigwa na Malaria ambayo siyo ya Kawaida.. kwa Jinsi nilivyokuwa Kila mtu alisubiri tu.. Nipelekwe Mortuary!.. Mungu akajalia Nikapona.. (Asante Mungu)

Case ya Mwisho Ambayo Mpaka leo inajirudia Kichwani Mwangu ni September 2009, Nadhani Nilikuwa Kidato cha kwanza, kuna mshikaji Mmoja hivi wa kitaa alikuwa kwenye 20's kiumri tulikuwa tunataniana nae sana.. hio siku amelewa wikiendi Moja Hivi.. Katika kutaniana Jamaa akamind na akataka kutupiga.. na alikuwa very serious, Mshikaji alikuwa Kashikilia Kipande cha Nondo 20mm, basi akatokea Baba Mmoja alikuwa Mbabe pale Kitaa, akataka kuamua.. Jamaa akaona kabla hatujaamuliwa sijui anipige na ile nondo.. ile ananipiga na Nondo nikainama ikampiga yule Baba Shavuni alizima hapo hapo na kulazwa Hospitali zaidi ya Miezi sita (Assume ingelikuwa Mimi na Nilikuwa Mtoto si Nishakufaa??)... sometimes nahisi nimemtoa huyo Baba Kafara!

Huwa Nikikumbuka hizi case Nabaki tu siamini Kama Hazikutoka na Roho yangu..

Je wewe mwanaJF ni cases gani Ambazo hutosahu zilizokaribia kuchukua Uhai wako??

Muwe na Usiku Mwema!


ALFRED
kwa maelezo yako nimegundua bado una umri mdogo. kama sijakosea wewe ni kijana uliyezaliwa mid 90s.

"uza mechi" kwanza kwa mademu 20 au zaidi halafu uje utupe tathimini yako ya kukwepa kifo.[emoji23]
 
Kwahiyo kifo kikikukosa mara 4 haufi mpaka zitimie hizo 6?

Sometimes Mungu hua anatoa mitihani ya maradhi na ajali kwa binadamu kama ukumbusho tu kua yeye yupo na anapaswa kuabudiwa,

Mara nyingi mitihani hii huwafika wale wote waliomsahau Mungu kwa Ibada,sadaka na mambo mengine mema.
Ni tathmini tu hizo mkuu sio perfect 100%
 
Mwaka 1996,Mimi, mama na bro wangu tuliumwa sana. Sijui ilikuwa nini..bro akafariki(RIP). Mi na bi mkubwa tukapona kwa dawa za kienyeji zile za kuvukiza.
Kila nikikumbuka naona kama ajabu kuwa hai leo hii.
Daah Poleni sana Mkuu, Kaka Apumzike kwa Amani.
 
Kifo kikikujia njia yako huwa hakina kona
Unapaswa kusema umekoswa kuingia kwenye majanga makubwa ya kuhuzunisha kwa neema za Mungu maana kuumwa mahututi sio dalili ya kifo wala kupatwa na gumu lolote
 
Kifo kikikujia njia yako huwa hakina kona
Unapaswa kusema umekoswa kuingia kwenye majanga makubwa ya kuhuzunisha kwa neema za Mungu maana kuumwa mahututi sio dalili ya kifo wala kupatwa na gumu lolote
Mkuu kuna wakati unaumwa hadi unasema Hapa siponi asee
 
Unamjua Fiedel Castro? Najua unamjua.....huyo ndiye gwiji la kukoswakoswa na kifo!!!
 
Tafiti za wadhungu na waafrika ziko tofauti walahi!
Uwongo mtupu!
 
Unamjua Fiedel Castro? Najua unamjua.....huyo ndiye gwiji la kukoswakoswa na kifo!!!
Bwana Castro inaaminika alikoswa na Kifo mara 562, Mungu Ampumzishe kwa amani
 
Back
Top Bottom