Tafiti Mpya: Mwili wa Binadamu hauhitaji wanga kabisa - (0%)

iArmaniAdamson

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
944
Reaction score
289
HII NI HABARI NJEMA KWA WASIOPENDA UNENE NA WANAOTAKA WASIPATWE MAGONJWA YA KISASA!

Kwa miaka sita iliyopita duniani tatizo la kisukari limeongezekwa kiasi cha asilimia 600%.

Wataalamu wamegundua kwamba, aina ya vyakula sasa hivi vina asilimia kubwa sana za wanga (Carbs) kuliko miaka ya zamani.

Dr. Sally Hallberg amesema kwamba tofauti na mazoea ya watu wengi, ugonjwa huu unasababishwa na mwanadamu kula wanga mwingi kuliko kiasi kinachohitajika mwilini.

mwanadamu anachohitaji zaidi ni Protini, Mafuta na Vitamini - kwa maana nyingine vyakula kama mchele/wali, mkate, pasta, pizza, viazi mviringo, noodles, ugali na mikate isiyotowa chachu (naan) ni VITU VYA KUEPUKA KABISA ili usipate tatizo hili.

Badala yake ule vyakula vyenye protini kubwa kama nyama na mayai, na pia ule mboga za majani nyingi zaidi na matunda, jambo zuri ni kwamba, kuna kiasi cha wanga pia kiko kwenye mboga za majani:-



 
Last edited by a moderator:

Pamoja na tafiti zenu zote, hamuwezi kukwepa ukweli kwamba watu wengi wanakula sana kuliko mahitaji ya mwili.
 
Last edited by a moderator:
Pamoja na tafiti zenu zote, hamuwezi kukwepa ukweli kwamba watu wengi wanakula sana kuliko mahitaji ya mwili.

ni kweli kabisa, ukiangalia tu kwa alafu, keki hizi na maandazi saizi zake ni kubwa sana kulinganisha zamani, mtu mmoja anakula maandazi sita asubuhi, au nusu lofu ya mkate au haya mabaga, unakuta kijana mdogo amemaliza shule anaanza kazi ananenepea kama nini.

Tatizo pia linachangiwa maisha ya sasa, wengi wamekaa kwenye computer, smart phone au TV, hakuna mazoezi alafu unakula chipsi na baga (burger) na jinsi unavyokula ndio mwili unachoka.

Ukweli ni kwamba mwili unachoka kushusha sukari kwasababu hauitaji, na sio mbali kisukari kinapanda na unaishi maisha ya tabu.
 
Mkuu iArmaniAdamson nimefuatilia mabandiko yako mengi na ninakukubali kwa hali ya juu sana.

Lakini kwa hili kidogo nimepata utata.

Huko kwetu nitokako watu miaka nenda miaka rudi wamekuwa wakila marundo ya ugali na vipande viduchu vya papa na mboga za majani. Ukienda Usukumani watu wanakula mamilima ya mabugali na kitoweo ni majani na manukuu machache ya nyama. Lakini kwote huko magonjwa ya sukari yalikuwa nadra sana mpaka hizi siku za karibuni.

Sasa kwa mtazamo wako hapa wanga unaelezeaje hii hali?

  • Sijui kama maisha ya kujibweteza nayo yanachangia hili tatizo la sukari.
  • Au pengine kwa sababu watu wanaishi maisha marefu siku hizi ndio maana haya matatizo yanajitokeza.

Maoni yako, please.
 

hilo neno sedentary ni gumu,
 
Last edited by a moderator:
Kama sedentary life style ni ile inayohusisha ulaji wa nyama na unywaji wa maziwa ni kweli ndio haswa chanzo kuongezeka unene na kisukari cha type1kuongezeka kwa zaidi ya mara 600 zaidi mzaziwa na nyama ndio haswa tatizo lakini kwa yoyote mwenye allergy ya kitu chochote zimeanzia kwenye unywaji wa maziwa.
 
Mimi ninahisi hilo nandiko la huyo jamaa linawahusu sana watu mjini kwasababu watu wa mjini wanakula vitu vingi sana harafu hawapati suruba yoyote kama mazoezi ili kutoa sumu mwilini
Na tena hili swala linawahusu sana waathilika kwasababu wanasema mtu ukiathilika ni lahisi sana kupata magonjwa kama hayo kwasababu mwili wako unakua hauna kinga.
 
Last edited by a moderator:
kisukari na magonjwa mengine mengi ya sasa yananakisi mabadiliko madogo ya gene zetu bila kusahau kukua kwa uchumi.
wanga unaweza kutengenezwa na mwili toka bidhaa nyingine zisizo na asili ya wanga, hivyo hauepukiki.
 

Inawezekana mkuu.
 

Sedentary nilimaanisha kujibweteza, kutofanya mazoezi au kazi za suluba na matokeo yake ni kuongezeka mwili/uzito. Samahani.

Naona umefafanua vizuri lakini sidhani kama nyama na maziwa vinachangia sukari. Mimi sio mtaalamu nipo hapa kujifunza. Asante kwa mchango.
 
Nenda YouTube andika Udderly amazing walter j veith utashangaa jinsi maziwa na nyama vilivyochangia watu wa kijijini kupata kisukari
 

Mkuu huko watu walikuwa wanakula dona, ss kl kona ni sembe hulioni hilo muheshimiwa?
 
Wanataka soko la bidhaa zao tu, walisema ukila uwe na matunda pembeni baadaye wakasema baada ya nusu saa tangu ule ndo ule matunda, hatuwaelewi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…