Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,830
- 972
Wanajamvi,
Kumekuwa na Upotoshaji mkubwa Kuhusu ubeberu na mabeberu wenyewe. Hili huenda linafanywa makusudi au kwa kutokujua.
Nilipokuwa shule ya msingi nilifundishwa kuwa ubeberu (imperialism) ni ubepari uliokomaa na kuvuka mipaka. Watu waliosoma kipindi changu wanakumbuka hili. Tafsiri hii ni tafsiri rahisi na nzuri.
Wanahistoria wanajua kuwa ukoloni haujaisha ila umebadili fomu kutoka kuwa ukoloni wa kiutawala, kijeshi na kiuchumi mpaka kuwa ukoloni mamboleo (neocolonialism). Njia kubwa ya kueneza ukoloni mamboleo ni kwa kupitia ubeberu.
Ubeberu upo zaidi kiuchumi, yaani baadhi ya matajiri (Filth billionaires) hasa kutoka nchi za magharibi na makampuni makubwa (multinational companies) ambao Wana nguvu ya kuweka viongozi madarakani hutawala uchumi wa dunia kupitia ubeberu hivyo hao ndio wanakuwa "mabeberu".
Ubeberu unatekelezwa zaidi Afrika kutokana na sababu nyingi ikiwemo ukweli kuwa Afrika ndio bara pekee lililobaki na rasilimali nyingi. rejee sababu za ukoloni: kutafuta masoko kwa bidhaa za viwanda vyao, malighafi kwa viwanda vyao, ardhi n.k, Mahitaji hayo yangali hai mpaka sasa. Lakini ubeberu pia unatekelezwa zaidi Afrika kutokana na ukweli pia baadhi ya viongozi wetu ni dhaifu dhhofu li hali huku wakiutukuza umagharibi na kuutweza uafrika wao.
Ili iwe rahisi kwa ubeberu kufanya kazi, kunapandikizwa viongozi vibaraka ambao hao wanakuwa ni "yes sir" mbele ya mabeberu. Akipatikana kiongozi imara ambaye hataki ujinga, huyu atapigwa vita na kusukiwa mipango ya kung'olewa kwani ni hatari kwa uchumi wa mabeberu. Kiongozi huyu ataitwa kila majina. Chukulia mfano ufuatao:
Uko bandari na unapiga dili zako na kila siku unakomba mshiko wa nguvu. Mara paap! anakuja meneja anakata na kuziba mirija you're ya rushwa na ize mane, utampenda? Lazima mtakaa kama kamati ya roho mbaya ili kuona jinsi ya kumshughulikia.
Sisi Kama nxhi tumeamua kulinda rasilimali zetu, hi maana yake ni kuwa tumetangaza vita ya kiuchumi. Kuishinda hii asiwadanganye mtu, Magufuli haiwezi peke yake. Ni lazima tuungane, tuwe wazalendo na kuweka maslahi ya Tanzania mbele.
Mabeberu wananguvu sana lakini wanatafuta chanzo kutoka ndani ya nchi. Tukiwa wamoja, hawawezi penya.
Nahitimisha kwa kusema sio kila utawala, nchi au kampuni za magharibi ni za kibeberu bali zile tuu zinazotenda ubeberu.
#ubeberuupotuwemacho
Amani Msumari
Tanga