Tafsiri ya kibonzo cha Kipanya kuhusu CHADEMA na mchoro wa pundamilia usiokwisha

Tafsiri ya kibonzo cha Kipanya kuhusu CHADEMA na mchoro wa pundamilia usiokwisha

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Wakuu,

Masoud Kipanya huwa anaongea kwa lugha ya picha na kuachia hadhira kutafsiri kutokana na uelewa wa kila mmoja.

Je, hii picha yenye viboksi vitatu, ikiwa na rangi za CHADEMA lakini pia kiboksi cha kwanza kikiwa kimechorwa sehemu ya nyuma ya Pundamilia inamaanisha nini?
Kipanya.jpg
 
Huyo pundamilia akionekana kwenye kibox Cha 3... Ujue Chadema imechukua Nchi
 
Wakuu,

Masoud Kipanya huwa anaongea kwa lugha ya picha na kuachia hadhira kutafsiri kutokana na uelewa wa kila mmoja.

Je, hii picha yenye viboksi vitatu, ikiwa na rangi za CHADEMA lakini pia kiboksi cha kwanza kikiwa kimechorwa sehemu ya nyuma ya Pundamilia inamaanisha nini?
View attachment 3224803
Hii kinaamanisha LISU na Lema wamo kiboksi cha 1, cha 2 na cha 3 hakina wanachama, wamewekewa wanaharakati
 
Huyu na ye ni wa kumpuuza tu... Asituumize kichwa. Toka atengeneza guta ya matairi manne na ya mafuta na kuiuza milioni 72 nilimdharau hapo hapo..
Hahahaaaaa
 
Masoud kipanya ni wa kupuuzwa katika michoro yake ya kisiasa haina uhalisia na ukweli zaidi uchekeshaji tu. Alichora kaburi la kuzikia chadema, chadema haikufa akachora hilo kaburi limejaa maji na kugeuka swimming poola kuna jibaba limo humo ndani limepozi kwenye hayo maji. Leo tena kachora bendera ya chadema inatoweka taratibu na pundamilia anaanza kujitokeza taratibu aonekane pahala pa bendera. Maoni yake hayana ukweli kwa kinachotokea kwa chadema
 
Back
Top Bottom