Tafsiri ya picha katika ulimwengu wa kiroho

Heshima kwako kiongozi [mention]Mshana Jr [/mention] .!? Najua kiongozi umebarikiwa mambo mengi katika udadavuzi wa ndoto kiroho. Leo nimeota naendesha baiskel lakini katika hiyo baiskel nimebeba maji nyuma na mbele amekaa kijana, safari ilikuwa ndefu kidogo lakini road yetu kulikuwa na watu wengi na baiskel yangu ilikuwa na break za kutosha hadi wa tembea kwa miguu wana sifia. nilifika sehemu kuna watu wengi sana lakini chini kuna tope la kutosha. Hii ndoto ina maana gani mkuu.!?
 

Msimu wa mvua huu mkuu. Itakuwa hivyo tu.
 
Angalia ndoto ya leo kisha kesho tuwasiliane
 
Angalia ndoto ya leo kisha kesho tuwasiliane

Ndoto ya leo kiongozi nimeota naogelea bahari tulivu yenye kina kirefu zaidi nilipo fika ufukweni kuna jamaa wakawa wanasema umeweza vipi kuogelea bahari yenye kina kirefu kiasi hiki. Mkuu ni mrejesho wa ndoto ya leo pia nipe maana halisi ya hizi ndoto [mention]Mshana Jr [/mention] Asante.
 
Ndoto zote mbili zina tafsiri moja tuu USHINDI.. kuna changamoto unazipitia lakini ziko ndani ya uwezo wako kwakuwa hakuna iliyokushinda hata moja, na kama kwasasa huna changamoto basi zinakuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…